Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:49

Idadi ya watu duniani yafikia bilioni 7


Idadi ya watu Duniani imefikia bilioni 7, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa
Idadi ya watu Duniani imefikia bilioni 7, kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa yatoa ripoti ya idadi ya watu duniani kufikia Jumatatu ambapo Afrika idadi inatarajiwa kukua mara tatu

Idadi ya watu Duniani imefikia bilioni 7 Jumatatu na kupelekea kuwepo na sherehe na wasi wasi wakati mmoja kutokana na namna watu zaidi wanavyo athiriwa na rasilimali ya dunia inayopungua. Umoja wa Mataifa ulichagua Octoba 31 kuwa siku ya kuadhimisha tukio hili la kihistoria.

Japokuwa ni vigumu kujua wakati ni mtoto gani anaezaliwa anafikisha idadi ya watu bilioni 7 Duniani, Ufilipino ilikuwa nchi ya kwanza kutangaza kuzaliwa kwa mtoto huyo. Danica May Camacho alizaliwa dakika chache kabla ya kuingia siku ya Jumapili katika hospitali moja huko Manila.



Sherehe pia zilifanyika India, nchi ambayo huwenda hivi karibuni ikaishinda China kama nchi yenye idadi kubwa ya wakazi Duniani.

Aidha kufikia idadi hiyo ya kihistoria ya watu bilioni 7 ni dalili ya kuonesha kwamba watu wanazidi kuishi maisha marefu na kuimarika kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa na wanaonusurika, wataalamu pia wanaonya juu ya mahangaiko yanayozidi kuzikabili idadi kubwa za watu kutafuta rasilimali ikiwa ni pamoja na chakula na maji.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wa idara ya idadi ya watu wanasema nchi nyingi zilizo kusini ya jangwa la Sahara zenye kipato kidogo na baadhi ya nchi huko Asia zimeshuhudia ukuaji wa idadi ya watu unaozidi kiwango cha ukuaji wa uchumi.

Idadi ya watoto wanaozaliwa katika nchi nyingi za Ulaya na Japan imeshuka chini ya kiwango cha watu wanaofariki na kusababisha wasi wasi kwamba upungufu wa kazi na uzalishaji kunaweza kutishia mwenendo wa maisha.

Kwa mujibu wa ripoti ya idadi za karibuni za Umoja wa Mataifa, idadi ya watu Duniani inakadiriwa kuvuka bilioni 9 kabla ya mwaka 2050 na kufikia bilioni 10.1 ifikapo mwishoni mwa karne, kama kiwango cha sasa cha kuzaliwa watoto kinaendelea kwenye viwango vilivyotarajiwa.

China hivi sasa ipo juu ikiwa na idadi ya watu bilioni 1.34, India inafuatia kwa watu bilioni 1.2. Idadi ya watu Afrika inatarajiwa kukua mara tatu zaidi na kufikia bilioni 3.6 mwanzoni mwa karne ijayo.

XS
SM
MD
LG