Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:52

UN yasema jeshi la DRC la changia ghasia


Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakipatiwa mafunzo ya matibabu na wanajeshi wa Marekani kutoka kikosi cha AFRICOM
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakipatiwa mafunzo ya matibabu na wanajeshi wa Marekani kutoka kikosi cha AFRICOM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumatatu inasema mitandao ya uhalifu katika jeshi ni sababu kuu ya mgogoro huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Ripoti ilisema baadhi katika jeshi wamejiunga na makundi ya uasi yenye silaha ili kunyonya rasilimali za asili za taifa hilo la Afrika ya kati. Wachunguzi walielezea mifano kadhaa ya wanamgambo kuchukua kinyume cha sheria madini na rasimali za asili, kukamata ardhi, kuwabaka wanawake, kuandikisha wanajeshi watoto na ujangili wa wanyama pori walio hatarini kutoweka.

Umoja wa Mataifa Jumatatu iliendeleza marufuku yake ya silaha dhidi ya watu na makundi ambayo hayahusiani na serikali ya DRC. Pia iliongeza marufuku ya kusafiri na vikwazo dhidi ya watu wanaohusishwa na makundi haramu.

Baraza la usalama pia lilisema kuwa mtu yeyote anayeingiza madini kutoka DRC itamchukulia hatua kuhakikisha fedha haziendi mikononi mwa magenge yenye silaha.

Mashariki mwa DRC imekumbwa na mapigano tangu mauaji ya halaiki nchini Rwanda mwaka 1994 yalipovuka na kuingia drc. Wanamgambo wa kihutu ambao walishiriki katika mauaji ya zaidi ya watusi 500,000 na wahutu wenye msimamo wa kadri walitafuta hifadhi huko DRC.



XS
SM
MD
LG