Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:17

UN yatayarisha jopo la uchunguzi DRC

Justine Masika Bihamba anapigana dhidi ya ubakaji unaofanyika huko DRC.
Justine Masika Bihamba anapigana dhidi ya ubakaji unaofanyika huko DRC.

Umoja wa Mataifa unasema unatayarisha jopo la maafisa wa ngazi za juu kusikiliza ushahidi kutoka kwa waathirika wa ubakaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, ambako maelfu wanabakwa kila mwaka.

Jopo hilo litaanza kukutana Alhamisi Septemba 30 katika mji wa Bukavu, mashariki mwa Congo na litasikiliza ushahidi kutoka kwa watu waliobakwa katika majimbo kadhaa hadi Oktoba 10.

Taasisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema mashahidi watazungumza kuhusu yaliyowapata na kuchangia mawazo yao kuhusu haki, tiba athari za kisaikolojia na huduma za jamii zilizopo kwa waathirika.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema wanapanga kujadili matokeo hayo Oktoba 12, kwenye kikao maalumu katika mji mkuu Kinshasa. Afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya ghasia za ngono, Margot Wallstrom, yupo Congo wiki hii.

Afisa huyo anakutana na maafisa wa DRC, Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wengine wa kutoa msaada wa kibinadamu huko Kivu Kaskazini.

XS
SM
MD
LG