Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:49

Ujumbe wa waasi wa Yemen watashiriki mazungumzo ya amani


Mvulana akipiga kelele akiwa amejipenyeza kwenye bendera ya waasi wa Kihouthi wakati wa maandamano dhidi ya shambulizi la anga lililofanywa na Saudia Arabia nchini Yemen.
Mvulana akipiga kelele akiwa amejipenyeza kwenye bendera ya waasi wa Kihouthi wakati wa maandamano dhidi ya shambulizi la anga lililofanywa na Saudia Arabia nchini Yemen.

Wajumbe kutoka kundi la waasi wa kihouthi nchini Yemen na washirika wao wanasema watashiriki mazungumzo ya Amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa nchini Kuwait, baada ya kukaa nyumbani kupinga shutuma za ukiukaji wa sitisho la mapigano kunakofanywa na majeshi yanayoiunga mkono serikali.

Wawakilishi kutoka pande zote wa-Houthi na chama cha rais wa zamani Ali Abdullah Saleh, ambacho kinawaunga mkono wa-Houthi, walisema wanapanga kuwasili nchini Kuwait leo Jumatano au kesho.

Umoja wa Mataifa ulijaribu kuanza mashauriano Jumatatu, lakini maafisa waliakhirisha mazungumzo kwa muda wakati wajumbe pekee wa serikali ndio waliwasili.

Baada ya kutangaza kuchelewesha mazungumzo, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Ismail Ould Cheikh Ahmed aliishukuru serikali kwa nia yake ya dhati na alisema anamatumaini wa-Houthi hawatakosa kuitimia fursa hii ili kuweza kumaliza ghasia nchini Yemen.

XS
SM
MD
LG