Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 11:12

Umoja wa mabunge dunia watoa ripoti


nembo ya UNDP
nembo ya UNDP

Wabunge mia sita na sitini kutoka mabunge 125 ulimwenguni kote walishiriki kwenye utafiti wa ripoti.

Raia wengi kwenye nchi mbali mbali ulimwenguni kote hawaamini mabunge. Hii ni kulingana na ripoti iliyozinduliwa jumatatu mjini Kampala na umoja wa mabunge ulimwenguni pamoja na shirika la umoja wa mataifa la UNDP. Wabunge kutoka bunge 159 ulimwenguni kote wamekuwa mjini Kampala kuanzia jumamosi kuhudhuria kikao cha 126 umoja wa mabunge ulimwenguni.

Ripoti inayoitwa " Sura inayobadilika ya uwakilishaji bungeni" inapendekeza wabunge kushirikiana kwa karibu na wapiga kura ikiwa watataka kuaminiwa na raia.

Wabunge mia sita na sitini kutoka mabunge 125 ulimwenguni kote walishiriki kwenye utafiti wa ripoti hii ambayo inalenga kuwasaidia wabunge na wanasiasa kwa ujumla kuelewa jinsi ya kuyashughulikia maswala ambayo yanawaathiri wapiga kura.

Rais wa umoja wa mabunge Abdelwahad Radi alisema ni dhiri kuwa wapiga kura hawatosheki kupiga kura tu, lakini wanataka kushirikishwa zaidi kwenye mipango yote ya demokrasia.

Rebeca Grynspan anafanya kazi na UNDP shirika lililochangia kwenye utafiti wa ripoti hii, amesema ingawa uchaguzi umeungwa mkono kwa kiasi kikubwa sana ulimwenguni kote, inafaa kuangalia ni vipi mabunge yataweza kukabiliana na mahitaji yanayoongezeka ya wapiga kura. Wapiga kura wanahitaji uchunguzi na uwajibikaji kutoka kwa wabunge na pia wanataka kushirikishwa.

Kwingineko, Misiri, Ufaransa, Uingereza, Imarat, umoja wa jumuiya za kiarabu na Canada tayari zimewasilisha ombi lao la kutaka usalama wa Syria ujadiliwe kwenye mkutano wa umoja wa mabunge kama jambo la dharura.

XS
SM
MD
LG