Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:46

Majeshi ya falme za kiarabu yajitoa vita ya Yemen


Wanajeshi wa Umoja wa Falme za Kiarabu
Wanajeshi wa Umoja wa Falme za Kiarabu

Umoja wa Falme za Kiarabu umetangaza kwamba wanajeshi wake hawatashiriki tena katika vita vya Yemen ambako vikosi vyake vilikua washirika wakuju mkubwa katika muungano uliokuwa ukiongozwa na Saudi Arabia katika mapambano na waasi wanaoungwa mkono na Iran kumalizika mwaka jana.

Taaarifa iliyotolewa katika lugha ya Kiarabu hata hivyo inasema vita hiyo kwa ujumla vimemalizika.

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje, Anwar Gargash, ilichapishwa tena kwenye Twitter na Mwanamfalme wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed bin Zayed Al-Nahyan, ambaye alichapisha tafsiri zote mbili kwenye akaunti yake rasmi.

Mwanamfalme huyo pia anahudumu kama naibu Kamanda Mkuu wa Falme za Kiarabu. Ingawa waasi wa kihouthi wameondolewa kutoka miji ya kusini ya Yemen, yanayoshikiliwa na wanajehsi watiifu na Rais Abdu Rabu Mansour Hadi lakini sehemu kubwa ya kaskazini na kati ya nchi hiyo inashikiliwa bado na waasi.

XS
SM
MD
LG