Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 08:59

Shirika la haki laomba kubuniwa kwa mahakama ya Uhalifu wa kivita Sudan Kusini


Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake hapa Marekani la 'Human Rights Watch' limeomba Umoja wa Afrika kubuni tawi la mahakama ya kitaifa ikiwa ni sehemu ya mkataba wa amani wa Sudan uliofanyika Agosti 2015 kwa nia ya kuhukumu washukiwa wa uhalifu wa kivita.

Mratibu wa program ya haki katika shirika hilo, Elise Keppler, amesema kubuniwa kwa mahakama hayo kutadhibitisha kuwa Umoja wa Afrika una ari ya kusitisha uhalifu wa kivita nchini Sudan na kwamba una nia ya kuwafungulia mashitaka waliotekeleza uhalifu huo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hilo limejiri wakati Rais wa Sudan Kusini Salva Kirr pamoja na makamu wake wa kwanza Riek Machar kutoa maoni ya maandishi kwenye gazeti la New York Times wakiomba dunia kuunda tume ya ukweli na maridhiano kama ile ya Afrika Kusini badala ya mahakama. Hata hivyo Keppler amesema hatua hiyo inaashiria kukwepa sheria kutoka kwa viongozi hao.

XS
SM
MD
LG