Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:35

Sera Mpya ya Trump Inaweza Kubadilisha Mahusiano ya Marekani Kimataifa


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump ameahidi mabadiliko makubwa katika sera ya mambo ya nje wakati wa kampeni, akieleza kusudio lake la kutafuta maeneo ya ushirikiano na Russia, na kuahidi kuchukua msimamo mkali dhidi ya Iran na China.

Rais pia aliahidi kumsaidia kwa nguvu zote kiongozi wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Mwandishi wa VOA amesema kuwa mwezi moja sasa akiwa katika nafasi yake ya urais, uongozi huo unajaribu kutafuta mwelekeo mpya.

Mwandishi wa VOA ameripoti kuwa katika hotuba yake ya kuapishwa Rais Donald Trump alisisitiza kuwa sera ya mambo ya nje ya Marekani lazima iongozwe na msingi mmoja.

“Kuanzia siku ya leo na kuendelea, itakuwa ni Marekani kwanza, Marekani kwanza. Hili litahusu kila uamuzi wa kibiashara, ulipaji kodi, na masuala ya mambo ya kigeni.”

Mwandishi ameelezea kuwa katika mwezi wake wa kwanza rais ameanza kutekeleza mabadiliko ya mila zilizokuwa zikitumika katika muongo mmoja na uhusiano wa Marekani kimataifa.

Trump hivi karibuni alimkaribisha Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu White House, ilikuwa ni ishara ya umoja unao adhimisha zama mpya katika ushirikiano wa Marekani na Israeli, ambao ulikuwa sio mzuri wakati wa utawala wa Barack Obama.

Kama mgombea, Trump aliahidi kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem na alikuwa akielekea kuwa mwenye kukubaliana na suala la ujenzi wa makazi huko Ukingo wa Magharibi.

Lakini kama rais, Trump aligusia kuwa “anatarajia” kuhamisha ubalozi, na akahimiza Israeli “iahirishe” upanuzi wa makazi.

Katika mkutano na waandishi, Trump alijitoa kabisa katika msimamo wa awali wa Marekani juu ya suluhisho la kuwepo mataifa mawili ya Israeli na Palestina.

Rais Trump amesema: “ Ninatarajia kuona mataifa mawili na taifa moja, na napenda kile ambacho pande zote watacho kubaliana.”

Trump aliahidi kuizuia Iran kufikia silaha za nyuklia, akikosoa makubaliano ya nyuklia ya 2015 yaliyofikiwa kati ya Tehran na mataifa sita yenye nguvu duniani akiita “Makubaliano yasioyofaa kabisa.”

Wakati wa Februari, Trump aliiwekea vikwazo Tehran kutokana na kufanya jaribio lake la kombora la masafa ya kati.

Rais ameongeza kusema: “ Na nitafanya juhudi zaidi kuzuia Iran isiweze kamwe kutengeneza, na ni kamwe, silaha za nyuklia.”

Trump amerejea mara nyingi kupendekeza kuwa mahusiano mazuri na Russia ni jambo zuri, hata kama ina mafungamano na Iran, na shutuma za kwamba iliingilia kati kuvuruga uchaguzi Marekani mwaka 2016.

Jambo hilo limewashtusha baadhi ya wabunge wa Marekani na washirika wa Ulaya.

Akiwa Brussels wakati wa wikiendi, makamu wa rais Mike Pence alijaribu kuwahakikishia washirika wa Ulaya juu ya msimamo wa Marekani kwa Russia.

Alisema Marekani itaendelea kuiwajibisha Russia, na kwa angalizo la rais Trump tutaendelea kutafuta nyanja mpya za ushirikiano jambo ambalo Rais Trump anaamini linaweza kupatikana.

Trump mara nyingi ameikosoa China wakati wa kampeni za urais, akiishutumu kwa kuhusika na kuyumbisha soko la pesa za kigeni.

“Hawajakuwa wakifuata kanuni, na nafikiri ni muda muafaka wataanza kufanya hivyo.”

XS
SM
MD
LG