Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:16

Homa ya Manjano yaua watu 21 nchini DRC


Wanafunzi katika chuo cha afya wakipatiwa chanjo ya kwanza ya homa ya manjano huko El Geneina, Darfur Magharibi.
Wanafunzi katika chuo cha afya wakipatiwa chanjo ya kwanza ya homa ya manjano huko El Geneina, Darfur Magharibi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) jana Jumatatu limeripoti kwamba takriban watu ishirini na moja wamekufa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na ugonjwa wa homa ya manjano, kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi jirani ya Angola.

Shirika hilo lilisema kwamba kufikia Machi 22, visa vipatavyo 151 vilikuwa vimeripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. WHO ilionya kuwa kutokana na wingi wa watu wanaosafiri kati ya mataifa hayo mawili, pamoja na kuwepo kwa mbu wanaoeneza viini vya homa hiyo, kuna uwazekano mkubwa wa kuambukizwa na kuenea kwa ugonjwa huo kwa haraka.

Mlipuko huo ulianza mwezi Desemba katika mji mkuu wa Angola, Luanda, na umeenea katika majimbo mengi nchini humo, huku visa 1,100 vikiripotiwa. Takriban watu 168 wamefariki kutokana na homa hiyo.

XS
SM
MD
LG