Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:56

Uganda yaitaka UN kutoa ushahidi wa ripoti kuhusu M23


Rais wa Uganda Yoweri Museveni (R) akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame (L).
Rais wa Uganda Yoweri Museveni (R) akisalimiana na Rais wa Rwanda Paul Kagame (L).
Serikali ya Uganda inasema ripoti ya Umoja wa Mataifa inayodai kuwa nchi za Uganda na Rwanda zinawasaidia waasi wa kundi la M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC haina msingi wowote. Uganda sasa inataka Umoja wa Mataifa itoe ushahidi wa kuonyesha kuwa kweli wanajeshi wake wapo mashariki mwa Congo wakiwasaidia waasi wa M23.

Ripoti hii ya Umoja wa Mataifa ambayo haijachapishwa rasmi na shirika hili ilichapishwa jumanne ya wiki hii na shirika la habari la Reuters. Inasemekana Uganda imekuwa ikiwasaidia waasi wa M23 ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja



Waasi hawa waliteka sehemu kubwa za mashariki mwa DRC na kabla ya kumalizika kwa wiki hii, waasi hawa wanatarajiwa kuwateuwa machifu watakao viongoza vijiji vya maeneo waliyoyateka.
Madai ya kuwa Uganda inalisaidia kundi la M23 hayakupokelewa vizuri mjini Kampala. Msemaji wa jeshi la Uganda, Kanali Felix Kulayigye alikanusha ripoti hiyo “kwanza kabisa hatujatuma majeshi ushahidi uko wapi ukiandika ripoti ya kiwango cha Umoja wa Mataifa ni lazima kuwepo na ushahidi, lakini watu kutembea tu sehemu fulani wakasikia fununu halafu wakaandika naona sio nzuri kwa Umoja wa Mataifa. La pili hawajajitahidi hata na kuuliza viongozi au wasemaji wa serikali au wa kijeshi kama mimi kwamba je tumesikia haya maneno je msimamo wenu ni vipi. Hamna hata kidogo, kwa hiyo hiyo ripoti sio ya ukweli.

Msemaji huyo wa jeshi la polisi alisema ni jambo la kuhudhunisha kuona ripoti kama hii ikichapisha na Umoja wa Mataifa. Alisema kuna watu wanaofanya kazi na Umoja wa Mataifa ambao hawataki usalama urejeshwe mashariki mwa Congo na sasa wameanza kusambaza fununu ili wazidi kuwa na ajira.

Kanali Kulayigye alisema hawana haja ya kwenda Congo kwa sababu “serikali ya Congo ilikubali Uganda kuwa mpatanishi wa upande zote mbili, na tunapozungumzia sasa hivi kuna viongozi wa M23 na viongozi kutoka Kinshasa hapa hapa ili waendeleze mazungumzo ya kutafuta suluhisho ya maswali ya mashariki mwa Congo na mkutano wa marais uliokaa hapa dhidi ya maswali ya Congo ulimruhusu Rais Yoweri Museveni kuwa mpatanishi wa upande zote mbili kwa hiyo tunashangaa kama Uganda kusikia tena kwamba hao wanaoitwa kwamba ni wataalamu wametokeza ripoti ya fununu bila ya ushahidi”.

Kulayigye anasema kati ya nchi zote za Afrika, Uganda inasifika kwa kuwa kwenye msitari wa kwanza wa kuhakikisha kuwa usalama unapatikana kwenye nchi zisizo na usalama.
XS
SM
MD
LG