Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:53

Uganda yafikisha mahakamani washukiwa wa mabomu


Washukiwa wa mabomu ya Uganda
Washukiwa wa mabomu ya Uganda

Mahakama moja nchini Uganda imewashtaki wakenya watatu kwa makosa ya ugaidi, mauaji na jaribio la kuua katika mashambulizi ya july 11 mjini kampala ambapo watu 76 waliuawa.

Mahakama moja nchini Uganda imewashtaki wakenya watatu kwa makosa ya ugaidi, mauaji na jaribio la kuua katika mashambulizi ya july 11 mjini kampala ambapo watu 76 waliuawa.

Hussein Hassa, Mohammed Adan Abdow na Idris Magondu walishtakiwa hivi leo katika mahakama ya hakimu mkazi katika mji mkuu Kampala.

Washtakiwa hawakutakiwa kujibu makosa na inatarajiwa watafikishwa tena mahakamani mwezi ujao.

Watu hao watatu walikuwa ni washukiwa wa kwanza kushtakiwa kwa mashambulizi ya mabomu, ambayo yalilenga mgahawa na klabu ambako watu walikuwa wamekusanyika wakiangalia fainali za kombe la dunia.

Maafisa wa Uganda wamewakamata takriban watu 20 kuhusiana na mashambulizi hayo. Kundi la wanamgambo wa kisomali la al Shabab lilidai kuhusika, na kusema walikuwa wakilipiza kisasi kwa kifo cha raia wa kisomali katika mikono ya walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia.

XS
SM
MD
LG