Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:31

Amri kuhusu kampeni yatolewa Uganda


Wagombea kiti cha rais Uganda Mbabazi na Kiza Besigye wakihudhuria katika moja mikutano nchini humo.
Wagombea kiti cha rais Uganda Mbabazi na Kiza Besigye wakihudhuria katika moja mikutano nchini humo.

Tume ya uchaguzi ya Uganda, imetoa amri inayopiga marufuku kufanya kampeni za kisiasa katika maeneo fulani, yakiwemo masoko, maeneo ya kuabudu na shule. Tume hiyo imewatahadharisha wale wanaowania urais nchini humo na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi wa Uganda kuhakikisha amri hiyo imezingatiwa.

Katika taarifa kwa waandishi wa habari, mwenyekiti wa tume hiyo, Badru Kiggundu, alisema hatua hiyo ni sambamba na maazimio yake ya awali kwamba tume hiyo ingeweka mikakati ya "kuhakikisha kwamba kuna usawa" huku nchi hiyo ya Afrika Mashariki ikielekea kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwaka huu.

"Tume ya uchaguzi imeshuhudia wawaniaji fulani wa urais wakienda kufanya kampeni mahospitalini. Tume hii ingependa kuwafahamisha wote kwamba si halali kufanya kampeni mahospitalini, kwenye msoko na hata shuleni," alisema Kigundu.

Lakini punde tu baada ya kutoa amri hiyo, wagombeaji wa urais kupitia vyama vya upinzani walilalamika vikali, huku baadhi yao wakisema kwamba tume hiyo inawabagua.

Kwa muda mrefu viongozi wa kisiasa nchini humo, akiwemo mpinzani mkali wa rais Museveni, Dk Kiza Besigye, wamekuwa wakifanya kampeni zao kwenye maeneo kama hayo yaliyopigwa marufuku.

XS
SM
MD
LG