Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:18

Jeshi la Uganda lategua kifaa cha mlipuko mjini Gulu.


Jeshi la Uganda UPDF na polisi wakifanya doria katika mji mkuu Kampala Uganda.
Jeshi la Uganda UPDF na polisi wakifanya doria katika mji mkuu Kampala Uganda.

Maafisa wa usalama nchini Uganda wametegua kifaa kinachoaminika kuwa ni bomu, kilichokuwa kimetegwa kwenye kituo cha mabasi kaskazini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Gulu karibu na mpaka na Sudan kusini.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Raia waligundua kifaa hicho Jumatatu mchana na kuwaita polisi pamoja na wanajeshi walikitegua kwa haraka bila kukikagua wakisema kwamba kilikuwa karibu kulipuka.

Wapelelezi nchini humo wanaendelea na uchunguzi wao wakisema kwamba mabaki ya vifaa yamepelekwa maabara kwa uchunguzi zaidi na kuwatafuta wahusika waliotega kifaa hicho kinachoaminika kama kingelipuka kingeweza kujeruhi au kuuwa watu walio mita hamsini za mraba kutoka pale kilipokuwa.

Mji wa Gulu unaopakana na Sudan Kusini ulishuhudia umwagikaji mkubwa wa damu wakati wa vita vilivyoongozwa na kundi la waasi la Lord’s Resisitance Army linaloongozwa na Joseph Kony.

XS
SM
MD
LG