Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:38

Ufaransa yaweza kushambuliwa tena na magaidi


Rais wa ufaransa Francois Hollande
Rais wa ufaransa Francois Hollande

Waziri mkuu wa ufaransa Manuel Valls ameonya Jumamosi kwamba Ufaransa inaweza kushuhudia mashambulizi zaidi kufuatia mashambuzlizi matatu ya kigaidi Ijumaa yaliyopiga nchi hiyo na pia Tunisia na Kuwait.

Viongozi wa dunia wameungana kupinga mashambulizi hayo , yaliyosababisha vifo vya dazani za watu kwa kupishana masaaa machache.

Kundi la Islamic state limedai kuhusika na shambulizi katika eneo la ufukwe la kitalii huko Tunisia ambalo limeuwa watu zaidi ya dazani tatu , wengi wakiwa watalii. Kundi hilo pia limedai kuhusika na shambgulizi la kujitoa muhanga kwenye msikiti wa wa- shia nchini Kuwait ambako zaidi ya watu 20 walikufa.

Huko ufaransa mshambuliaji aliingiza gari lake kwenye kituo cha mafuta cha kampuni ya Marekani na baadae kumuuwa mfanyabiashara .

Maafisa wa usalama wanasema mtuhumiwa amekamatwa. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- Moon amesema wale wanaohusika dhidi ya matukio hayo ya ghasia lazima wafikishwe mbele ya sheria.

XS
SM
MD
LG