Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:15

Uchunguzi wa ndege ya Malaysia iliyotoweka waendelea


Ndege ya shirika la ndege la Malaysia
Ndege ya shirika la ndege la Malaysia

Uchunguzi umeanza kubaini utambulisho wa abiria wanne waliokuwa ndani ya ndege ya Malaysia iliyotoweka ambao walikuwa na pasi za kuiba na stakabadhi nyingine bandia.

Waziri wa uchukuzi wa Malaysia anasema uchunguzi umeanza kubaini utambulisho wa abiria wanne waliokuwa ndani ya ndege ya Malaysia iliyotoweka, ambao walikuwa na pasi za kuiba na stakabadhi nyingine bandia.

Waziri huyo wa uchukuzi Hishammuddin Hussein aliwaambia waandishi habari Jumapili kuwa idara za kijasusi za Malaysia zinapeleleza orodha ya abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo na kushirikiana na wenzao wa kimataifa ikiwemo idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya Marekani FBI.

Maafisa wanasema pia kuwa kifaa cha ufuatiliaji wa safari za ndege kinaashiria ndege hiyo ilirudi nyuma badala ya kuendelea na safari yake kabla ya kutoweka. Timu za uokozi bado zinaendelea na juhudi za kuitafuta ndege hiyo.
XS
SM
MD
LG