Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:33

Uchaguzi unafanyika kwa mifarakano Mashariki ya DRC


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akipiga kura yake katika kituo cha kura mjini Kinshasa
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akipiga kura yake katika kituo cha kura mjini Kinshasa

Wapigaji kura walijitokeza kwa wingi Jumatatu, katika kila pembe ya DRC kushiriki katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi kutayarishwa na Wakongo wenyewe tangu uhuru

Mamilioni ya wa-Kongo walipiga kura zao Jumatatu katika uchaguzi wa pili wa vyama vingi tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kulikuwepo na ripoti za ghasia na tuhuma za wizi wa kura katika baadhi ya miji mikubwa ya Kongo, hata hivyo upigaji kura unaonekana umefanyika kwa amani katika maeneo mengi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Scott Stearns, akiwa Kinshasa anaripoti kwamba, polisi walifyetua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu walokua wanalalamika kwamba, wamegundua badhi ya karatasi za kura zimeandikwa tayari ili kumunga mkono rais Joseph Kabila.

Huko Goma, mwandishi wa VOA Ruben Lukumbuka, anaripoti kwamba wapigaji kura wengi hawakuona majina yao kwenye daftari ya wapigaji kura na kusababisha kuzuka mtaharuk katika vituo vya kupiga kura.

Katika mji wa Lumbumbashi watu wasojulikana walishambulia kituo cha kupiga kura kwa bunduki na kuwauwa polisi wawili kabla ya kutia moto sanduku za kutia kura.

Matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa Disemba 5 siku moja kabla ya muhula rasmi wa rais Kabila kumalizika. Kabila amekua madarakani tangu 2001 baada ya kuchukua uwongozi wa nchi kufuatia kuuliwa kwa babake Laurent Kabila.

XS
SM
MD
LG