Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:03

Tutokomeze ubaguzi dhidi ya Ukimwi:Aung San Suu Kyi


Wanafunzi wa shule ya sekondari Korea Kusini wajiopanga na kuonesha nembo ya kuhamasisha Ukimwi
Wanafunzi wa shule ya sekondari Korea Kusini wajiopanga na kuonesha nembo ya kuhamasisha Ukimwi
Ikiadhimisha siku ya Ukimwi Duniani Disemba Mosi 2013, Idara ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia HIV/Ukimwi UNAIDS ikishirikiana na mshindi wa tunzo ya Amani ya Nobel Aung San Suu Kyi wamezindua kampeni ya kutokomeza ubaguzi kwa kutoa wito kwa kufanyika mageuzi kote duniani.

Akizungumza mjini Melbourne Australia kudhimisha siku hii ya kimataifa Aung San Su Kyi amesema "nina amini katika dunia ambayo kila myu anaweza kuchanua kama ua. basi sote tunaweza kuleta mabadiliko kwa kuwaruhusu watu kustawi katika maisha yenye heshima bila ya kujali asili yao au wao ni nani. Ninamkaribisha kila mtu kunyosha mkono, kua na imani na kukomesha ubaguzi".

Bi Aung San Suu Kyi pamoja na mkurugenzi mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe walitangaza kampeni ya Kutokomeza Ubaguzi, Zero Discrimination kama kauli mbiyu ya mwaka huu pia.

Idadi ya vifo kutokana na Ukimwi, 2005-2012
Idadi ya vifo kutokana na Ukimwi, 2005-2012

Dk. Sidibe amesema "tunafahamu hatuwezi kufikia kiwango cha kutokuwa na uambukizaji mpya wa HIV na vifo vinavyohusiana na Ukimwi, bila ya kufikia lengo la kutokomeza ubaguzi"

Siku hii ysa leo ni muhimu katika kuwakumbusha watu wote dunaini kwamba ugonjwa huo haujapata bado tiba, kwa kufanyika sherehe na matukio mbali mbali katika pembe zote za dunia kuwahamasisha watu juu ya hatari ya janga hili.

Kulingana na takwimu za mwaka 2012 UNAIDS takriban watu milioni 35.3 kote duniani wanaishi na HIV, watu milioni 2.3 waliambukizwa upya na HIV na watu milioni 1.6 wamefariki kutokana na magonjwa yanayohusiana na Ukimwi.
XS
SM
MD
LG