Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 13:07

Uongozi wa Trump Kutumia 'Fursa Yoyote Itakayo Jitokeza' Kuzuia Wahamiaji


Rais Donald Trump (kulia) akiongea na waadishi wa habari waliokuwa ndani ya ndege ya rais. Pembeni ya Rais ni mkewe Melania.
Rais Donald Trump (kulia) akiongea na waadishi wa habari waliokuwa ndani ya ndege ya rais. Pembeni ya Rais ni mkewe Melania.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema bado anafikiria kutoa “amri mpya kabisa” inayohusu uhamiaji baada ya Mahakama ya Rufaa kwa kauli moja kupinga amri yake inayowazuia wakimbizi na raia wa nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Trump amewaambia waandishi wa habari akiwa katika ndege ya rais, Air Force One, Ijumaa kuwa amri mpya ya kiutendaji inaweza kutolewa mapema Jumatatu au Jumanne, iwapo uongozi wake utafikia uamuzi wa kuchukuwa hatua hiyo.

Amesema kuwa hatua hii inaweza kuwa ya haraka kuliko kupambana na maamuzi yaliyokwisha tolewa na mahakama. “Tunatakiwa kuharakisha kwa sababu za kiusalama,” amesema.

Mkuu wa wafanyakazi ikulu ya Marekani, Reince Priebus amewafafanulia waandishi, kuwa “kila njia mbadala ya kukabiliana na uamuzi huu ipo tayari, ikiwemo kukata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya mahakama ya rufaa, pamoja na kupambana na kesi hii kwa hoja zenye nguvu.”

Wakati huo huo, jaji ambae hakutajwa jina lake kutoka Mahakama ya Rufaa ameomba majaji 25 wa kudumu wa mahakama hiyo kupiga kura iwapo amri ya muda ya kusitisha katazo la rais (amri ya kiutendaji) lisikilizwe tena kabla ya jopo la majaji 11, kwa mujibu wa amri ya mahakama. Pande zote mbili katika kesi hii pia zimetakiwa kuwasilisha muhtasari wa maombi yao iwapo wanakubali shauri hilo wiki ijayo.

Mapema Ijumaa, Trump alisema alikuwa “hana shaka” kwamba wanasheria wa serikali wataweza kuushinda uamuzi uliokwisha tolewa na mahakama ya rufaa.

Hivi sasa wageni wasafiri waliokuwa na viza halali wanaweza kuingia Marekani bila kizuizi chochote.

XS
SM
MD
LG