Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 10:49

Trump ateuwa waziri wa Usalama wa Ndani


 Gen. John Kelly akizungumza na wanahabari kwenye jengo la Pentagon Jumatano
Gen. John Kelly akizungumza na wanahabari kwenye jengo la Pentagon Jumatano

Maafisa kutoka timu ya mpito wamesema kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteuwa Jenerali mstaafu kutoka kikosi cha Marines John Kelly kama waziri wa Usalama wa Ndani.

Maafisa kutoka timu ya mpito wamesema kuwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteuwa Jenerali mstaafu kutoka kikosi cha Marines John Kelly kuongoza wizara iliotatizika ya Usalama wa ndani yenye jukumu la kukabiliana na ugaidi na kutekeleza ahadi ya Trump ya kukabiliana na uhamiaji haramu.

Wameongeza kuwa Kelly amependekezwa kutokana na uzoefu wake kuhusu mpaka wa Marekani na Mexico na pia ari yake ya kukabiliana na madawa ya kulevya, ugaidi na tishio nyinginezo zinazoaminika kutoka mataifa ya marekani ya kati na kusini.

Mwaka wa 2010, mwanaye Kelly Liuteni Robert Kelly aliuwawa kwenye mlipuko wa ardhini nchini Afghanistan na kumfanya afisa wa ngazi ya juu zaidi kwenye jeshi la Marekani kupoteza mwana kwenye vita vya Afghanistan na Iraq.

XS
SM
MD
LG