Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 11:37

Msaidizi wa Trump asema Rais-mteule hatafuatilia uchunguzi dhidi ya Clinton


FILE - Hillary Clinton akizungumza New York, Nov. 9, 2016.
FILE - Hillary Clinton akizungumza New York, Nov. 9, 2016.

Msaidizi mmoja mkuu wa Rais-mteule wa Marekani Donald Trump amesema Jumanne kuwa kiongozi huyo hana nia ya kuendeleza uchunguzi zaidi dhidi ya Hillary Clinton na matumizi yake ya barua pepe, licha ya kuahidi wakati wa kampeni kuwa "atamweka jela."

Kellyanne Conway, ambaye sasa ni mshauri wa Trump baada ya kufanya kazi kama meneja wake wa kampeni, aliliambia shirika la habari ya MSNBC kuwa Trump "hana nia ya kuendeleza madai hayo."

Wakati wa miezi kadha ya kampeni, Trump kama mgombea wa chama cha Republican alishambulia jinsi Clinton alivyotumia hati zinazohusiana na usalama wa taifa katika mfululizo wa barua pepe wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje kutoka mwaka 2009 hadi 2013, huku wafuasi wake wakipiga kelele za "mfunge!" Wakati fulani Trump alisema kuwa endapo atachaguliwa, atateua mwendesha mashitaka maalum kumchunguza Clinton.

Katika mahojiano, hata hivyo, Conway alisema, " nafikiri Hillary Clinton bado anakabiliwa na ukweli kwamba sehemu kubwa ya Wamarekani wanamwona haaminiki, lakini kama Donald Trump anaweza kumsaidia, basi huenda hilo ni jambo zuri."

Matumizi ya Clinton ya mfumo wake binafsi wa barua pepe uliokuwa nyumbani kwake New York ilikuwa jambo kubwa katika kampeni, huku utafiti ukionyesha kuwa wapiga kura wengi walikuwa na shaka na maelezo yake kuhusu maelfu ya barua pepe alizotuma au kupokea alipokuwa mwanadiplomasia mkuu wa nchi.

Picha hii ya March 12, 2012, inamwonyesha Waziri Clinton wakati huo akisoma barua pepe katika simu.
Picha hii ya March 12, 2012, inamwonyesha Waziri Clinton wakati huo akisoma barua pepe katika simu.

Clinton alisema alitumia mfumo huo ambao haukuwa na kinga kwa sababu ilikuwa rahisi kwake kufanya hivyo kuliko kupitia katika mfumo wa serikali.

Uchunguzi wa FBI

Idara ya Uchunguzi ya FBI ilianzisha uchunguzi mrefu na kukuta baadhi ya nyaraka za siri katika barua pepe hizo, lakini mwezi Julai FBI ilisema ingawa Clinton hakuwa mwangalifu, hakuna makosa ya jinai aliyofanya. Trump aliendelea kumshambulia Clinton kuhusu swala hilo la barua pepe.

Halafu, siku 11 kabla ya uchaguzi wa Novemba 8, mkuu wa FBI James Comey alitatangaza kuwa wanachunguza sehemu nyingine ya barua pepe baada ya nyingine zipatazo laki moja kugundulika katika kompyuta ya mume wa zamani wa msaidizi wa Clinton Huma Abedin.

Lakini siku tisa baadaye, ikiwa siku mbili tu kabla ya uchaguzi, Comey akatangaza kuwa uchunguzi huo haujaona lolote jipya na hivyo kufunga uchunguzi huo.

Msaidizi wa Clinton, Huma Abedin
Msaidizi wa Clinton, Huma Abedin

Baada ya Uchaguzi

Siku baada ya ushindi usiotazamiwa wa Trump, Clinton na Wademocrat wengine walimlaumu Comey kwa kufungua uchunguzi mpya bila kutazamia siku chache kabla ya upigaji kura.

Wachambuzi wa siasa Marekani, hata hivyo, wanasema kushindwa kwa Clinton kuwafikia wazungu wa tabaka la wafanyakazi hasa katika maeneo ya kati ya nchi yenye viwanda ilikuwa moja ya sababu kubwa ya kushindwa.. Clinton alishindwa katika majimbo kadhaa ambayo Rais Obama alishinda katika chaguzi mbili na ilitazamiwa majimbo hayo yangempigia kura Clinton.

Trump ataapishwa kuwa rais January 20 huku Obama akiondoka madarakani.

XS
SM
MD
LG