Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:57

Ecuador inaendelea kuwatafuta waathirika wa tetemeko la ardhi


Jamaa waliopoteza ndugu zao katika tetemeko la ardhi la Portoviejo, Ecuador.
Jamaa waliopoteza ndugu zao katika tetemeko la ardhi la Portoviejo, Ecuador.

Timu ya uokozi nchini Ecuador inaendelea kuwatafuta katika vifusi walionusurika kwenye tetemeko la ardhi lililokuwa la kiwango cha 7.8 kwa kipimo cha rikta, huku mazishi yakianza kwa zaidi ya watu 500 waliokufa.

Idadi ya vifo inaonekana kuongezeka na baadhi ya maafisa wanasema zaidi ya watu 1,700 bado wamepotea ikiwa ni siku tatu baada ya tetemeko la ardhi la awali.

"Tuna watu 2,000 walioorodheshwa wanaotafutwa lakini mpaka sasa tumepata watu 300", naibu waziri wa mambo ya ndani wa Ecuador, Diego Fuentes, amewaeleza waandishi wa habari. Hata hivyo, wizara ya ulinzi ya Ecuador inaweka idadi ya watu waliopotea ni 231. Kwa mujibu wa makadirio ya serikali, zaidi ya watu 4,600 walijeruhiwa.

XS
SM
MD
LG