Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 11:20

Thamani ya Shilingi ya Tanzania yashuka


Soko la mboga na Matunda
Soko la mboga na Matunda

Dola moja ya Marekani yabadilishwa kwa shilingi zaidi ya 1,700Tanzania

Uchumi wa dunia unazidi kudorora na gharama ya maisha kupanda kila siku. Katika nchi nyingi zinazoendelea maisha yamekuwa ghali mno kwa watu wa kipato cha chini kuweza kumudu maisha.Huko nchini Tanzania hali si tofauti kwani thamani ya shilingi ya Tanzania imezidi kushuka kufikia Jumatatu dola moja ya kimarekani ilibadilishwa kwa zaidi ya shilingi elfu moja na mia saba.

Sarafu hiyo ya Tanzania imekuwa ikiyumba kwa wiki kadha sasa na kuwaathiri zaidi wananchi wa kawaida na hususan wafanyibiashara wadogo ambao pia wanalalamika kutokana na uhaba wa umeme. Hussein Kamote ni mkurugenzi wa shirikisho la wenye viwanda nchini humo na anasema kushuka kwa thamani ya sarafu hiyo kumeathiri sana wazalishaji. Hali hiyo pia imesabaisha wafanyibaishara kuongeza bei za bidhaa zao ili kupata faida kiasi kutokana na gharama kubwa ya ununuzi wa mali ghafi.

Bwana Kamote anasema haoni njia rahisi ya kutatua taizo hilo kwani imekuwa vigumu kupata na kuuza dola ya kimarekan.Tatizo lingine linalojitokeza nchini Tanzania ni ununuzi wa bidhaa kwa kutumia shilingi ya Tanzania na dola ya kimarekani kana kwamba zote ni sawa. Mchumi na mwanasiasa Hamad Rashid anasema hili limeathiri sana thamani ya shilingi nchini humo.Tatizo la kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania pia linalaumiwa kwa matumizi mabaya ya sarafu hiyo.

Na ingawa nchi zote za Afrika Mashariki zina tatizo sawa na hilo la kushuka kwa thamani ya sarafu zao bwana Rashid anasema hali nchini humo ni tete na kwamba tahamni ya shilingi yake imeshuka kwa kiwango kikubwa zaidi na kuwashtua wabunge na wafanyibaishara. Aidha Rashid anasema serikali ya Tanzania japo imelizungumzia swala hilo ilichukuwa mwendo wa pole mno kuweza kunusuru hali kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG