Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:08

Tetemeko la ardhi latokea Ecuador


Tetemeko la ardhi lenye nguvu za 6.7 kwenye kipimo cha rikta limetokea katika mwambao wa Ecuador mapema leo, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kutokea tetemeko baya la ardhi katika eneo hilo hilo.

Hakuna maafa yaliyoripotiwa na hakuna hatari ya kutokea tsunami, kwa mujibu wa ujumbe wa Twitter ya Rais Rafael Correa.

Nacho kituo cha tahadhari ya tsunami cha Pacific kimeleza pia kwamba hakuna dalili za kutokea kwa tsunami. Kukatika kwa umeme kumetokea na watu walikimbilia mitaani mara baada ya kuhisiia tetemeko hilo mjini Muisne, mji wa karibu na kitovu cha tetemeko kwa mujibu wa mashuhuda.

Tetemeko la nguvu za 7.8 kwenye kipimo cha rikta la mwezi Aprili mwaka huu lilikuwa baya katika kipindi cha miongo saba, na kusababisha vifo vya watu 650 na kujeruhi watu wengine 12,500 katika mwambao wa bahari ya Pacific.

XS
SM
MD
LG