Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:32

Kenya kuboresha mtandao wa Wi-Fi


Nguzo ikiwa imeshikilia nyaya za umeme Nairobi, Kenya.
Nguzo ikiwa imeshikilia nyaya za umeme Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa ripoti iliotolewa na serikali ya Kenya kupitia nyaraka kwa jina Telecompaper, Kenya inajitahidi kukamilisha kilomita chache za nyaya za kimitandao za optic fibre kwenye kaunti zote 47 ikiwa hatua ya kuimarisha mtandao wa Wi-Fi.

Kwa mujibu wa IT News Africa ripoti hiyo imebaini kuwa waziri wa utangazaji na mawasiliano, Sammy Itemere amesema kuwa kuna mpango wa kuishirikisha serikali kuu na serikali za kaunti kwenye ufunguzi wa angalao vituo vitatu nchini vya kurushia miale ya Wi Fi kwa umma.

Itemere pia amesema kuwa Serikali itashirikisha sekta binafsi katika kuimarisha miundo mbinu itakayopelekea upatikanaji wa uchumi wa kidijitali. Waziri huyo pia amesema kuwa kupitia ripoti ya Telecom Paper, serikali imeanza kutathmini sera za teknolojia ya habari za mitandao ICT, ikiwa njia moja ya kuielekeza nchi kwenye uchumi wa kidijitali.

Ripoti hiyo imefichua kuwa chini ya mpango wa kitaifa wa ICT wa 2013-2018, Serikali inakusudia kuorodhesha ICT kama sekta huru ya kiuchumi inayonuiya kutengeneza ajira na kuchangia mapato ya kiuchumi kwa asilimia 8. Amesema Serikali pia inaongeza juhudi za kuendeleza wataalam wa ICT wenye ujuzi wa hali ya juu. Wataam hao wanatarajiwa kuinua sekta ya ICT hadi kwenye viwango vya ushindani wa kiuchumi.

Wakati huo huo, kampuni ya teknologia ya Hauwei tawi la Uganda imetia saini mkataba na wizara ya teknologia ya ICT wakati wa sherehe zilizofadhiliwa na kampuni hiyo kwenye hoteli ya Serena, mjini Kampala. Mkataba huo unanuiya kutoa mafunzo ya kiteknologia kwa Serikali, taasisi za kielimu na kwa umma kupitia warsha zitakazo hamasisha umma kuhusu teknologia.

Waziri wa ICT wa Uganda, John Nasasira, amesema wizara yake itanufaika kutokana na ujuzi mkubwa na utafiti wa kiteknoligia uliofanywa na kampuni ya Hauwei. Mkurugenzi mkuu wa Hauwei tawi la Uganda, Stanley Chyn, amesema kampuni yake inanuia kufanya kazi kwa ushirikino na wizara husika katika maswala ya teknologia.

XS
SM
MD
LG