Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 19:20

Tekinolojia yasaidia kutoa chanjo


Simu ya mkononi
Simu ya mkononi

Sms zasaidia wazazi kupeleka wanao kwa chanjo

Kutuma jumbe fupi au sms kumekuwa mazoea hivi kwamba wengi huchukuliwa kuwa jambo la kawaida tu. Sasa, teknolojia hii inawapa watu njia mpya ya kuokoa maisha ya watoto wao. Daktari Mmarekani amefanyia majaribio mbinu ya kutumia jumbe fupi kukumbusha wazazi wapeleke watoto wao wakapewe chanjo dhidi ya homaya Influenza - ugonjwa unaoweza kuua. Shirika la Afya Duniani-(WHO)linasema kuwa influenza husababisha vifo vya watu nusu milioni kila mwaka. Ni ugonjwa hatari sana hasa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.Katika dunia iliyo na watu bilioni saba, takwimu za sekta ya mawasiliano zinaonyesha kuwa takribani watu bilioni sita wana simu za mkononi. Katika mataifa yanayoendelea, wahudumu wa afya katika maeneo ya mashambani hutumia simu za mkononi kuwasiliana na madaktari ili kupata maagizo kuhusu jinsi ya kutunza wagonjwa. Watafiti wa Marekani walijiuliza iwapo kutumia simu za mkononi kutuma jumbe za kukumbusha wazazi kuhusu chanjo za watoto wao kungewezesha watoto zaidi kulindwa dhidi ya homa ya Influenza na kupunguza visa vya wengi kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa huo. Daktari Melissa Stockwell aliongoza utafiti kuhusu mbinu hiyo. Anasema walitaka kujua iwapo watoto wa wazazi ambao wangetumiwa jumbe fupi za simu za mkononi wangekuwa katika nafasi bora ya kupata chanjo dhidi ya Influenza kuliko wa wazazi ambao hawakutumiwa jumbe hizo. Daktari Stockwell aliongoza shughuli ya kufanyia majaribio mbinu hiyo kwa kutumia watoto zaidi ya 9,000 walio chini ya umri wa miaka 18. Watoto walioshirikishwa katika utafiti huo waliteuliwa bila mpangilio maalumu. Kundi moja la wazazi lilipokea tu ukumbusho wa chanjo za watoto wao kupitia ujumbe wa sauti kwa simu wakaelezwa jinsi ya kupata vikatarasi vya maelezo kuhusu homa ya Influenza. Kundi jingine lilipokea ujumbe mfupi wa simu za mkononi ukiwaelezea kuhusu kirusi cha ugonjwa huo na umuhimu wa chanjo - walikumbushwa pia kupeleka watoto wao wakapate chanjo. Katika ujumbe huo mfupi wa simu za mkononi, Daktari Stockwell alitaka kufafanua mitazamo fulani mibaya kuhusu kirusi cha ugonjwa wa Influenza ulioshikiliwa na watu wengi. Aligundua kwamba wazazi ambao walipata jumbe fupi za simu za mkononi wangepeleka watoto wao kupewa chanjo kuliko wazazi ambao walipata ujumbe wa sauti tu kwa simu.Watafiti waliridhika na matokeo ya shughuli hiyo kwani yalionyesha kuna matumaini ya mbinu ya jumbe fupi kufanikiwa kukabili ugonjwa wa Influenza. Walisema mbinu hiyo ikitumika kote nchini, hatimaye watoto wachache zaidi watalazwa hospitali na wengine milioni mbili na nusu watakuwa katika bukheri wa afya.

XS
SM
MD
LG