Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:54

Tarehe ya uchaguzi yazusha malumbano Kenya


Riot police detain an anti-gay protester during an authorized gay rights rally in St. Petersburg, Russia.  A gay rights rally has ended in scuffles after several dozen protesters were confronted by about 200 conservative and religious activists. 
Riot police detain an anti-gay protester during an authorized gay rights rally in St. Petersburg, Russia.  A gay rights rally has ended in scuffles after several dozen protesters were confronted by about 200 conservative and religious activists. 

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi, IEBC anasema wako tayari kukubaliana na tarehe itakayoamuliwa na mahakama ya rufaa

Wanasiasa wa vyama mbali mbali huko Kenya wametoa maoni yanayotafautiana mwishoni mwa wiki baada ya Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC, Issack Hassan kutangaza Jumamosi kwamba uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 4 Machi 2013.

Waziri Mkuu Raila Oginga aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wa hadhara huko magharibi ya nchi kwamba hakuna anetaka uchaguzi wa 2013, bali wako tayari kwa uchaguzi wa Disemba 2012.

Wagombea wengine wenye matumaini ya kugombania kiti cha rais, William Ruto na Kalonzo Musoyka waliungana na Odinga na kutaka uchaguzi ufanyike mwezi wa Disemba.

Naibu waziri mkuu Musalia Mudavadi kwa upande wake alisema itakua bora kwa tume kujitayarisha inavyohitajika kuhakikisha uchaguzi ni wa huru na wa haki badala ya kutaka uchaguzi ufanyike mapema. waziri wa Utali Najib Balala ambae pia ni mwanachama wa ODM cha waziri mkuu anaunga mkono terehe ya Machi 4.

Akizungumza na sauti ya Amerika mchambuzi wa masuala ya kisiasa wakili Wanyiri Kihoro, akiungana na maoni ya baadhi ya wanasiasa alimtaka Bw. Odinga ajiuzulu mwezi Oktoba ili kumlazimisha rais kuitisha uchaguzi ifikapo mwezi Disemba.

Tume ya uchaguzi imetoa pia tarehe ya Disemba 17 ikisema itakua tayari kutayarisha uchaguzi wakati wowote pale afisi ya rais, bunge na mahakama watakapokubaliana.

XS
SM
MD
LG