Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:48

Wafanya biashara wa viumbe pori hai Tanzania “wamlilia” Magufuli


Rais wa Tanzania John Magufuli.
Rais wa Tanzania John Magufuli.

Nchini Tanzania Wafanyabiashara wa viumbe pori hai wamemuomba Rais John Mugufuli asikie kilio chao na kufungulia biashara yao ya kusafirisha viumbe hao nje ya nchi baada ya serikali kupiga marufuku usafirishaji huo tangu mwanzoni mwa mwaka huu

Wafanyabiashara hao walivamia Wizara ya Maliasili na Utalii na kuonana na Waziri mwenye dhamana Prof.Jumanne Maghembe kuhusu kilio chao hicho cha kutaka serikali ifungulie biashara yao ya uuzaji wa viumbe pori hai nje ya nchi

Kuanzia Machi 17 mwaka huu, Serikali ilisimamisha ghafla usafirishaji wa viumbe pori hai nje ya nchi, hatua iliyokuja baada ya wafanyabiashara hao kulipia gharama zote wizarani ikiwemo vibali, hivyo wametaka rais kuingilia kati jambo hilo.

Akizungumza kuhusu sakata hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe amesema kimsingi Serikali imepiga marufuku biashara ya kusafirisha viumbe pori hai nje ya nchi.

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe amesema “serikali imekataza kwa angalau miaka mitatu biashara hii iachwe ili idara ya wanyamapori ijipange namna ya kufanya biashara hii kwa usalama, uhakika na kwa kufuata sheria na sababu kubwa za serikali kuchukua hatua hiyo ni kwanza wanyama wa Tanzania wanakamatwa katika bandari na viwanja vya ndege vya nje ya nchi wakiwa hawakufuata taratibu za kusafirishwa.”

Hata hivyo waziri Maghembe amesema wataalamu wa wizara wanaendelea na uhakiki wa vibali vya wafanyabiashara hao ili wajue namna ya kuwalipa kifuta jasho.

XS
SM
MD
LG