Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:19

Tanzania: Mabadiliko makubwa katika uwongozi wa CCM


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akitowa hotuba mjini Dar es Salaam
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete akitowa hotuba mjini Dar es Salaam

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Jumatatu itakutana kupendekeza majina na kuchagua viongozi wa Sekretarieti na kamati kuu ya chama hicho ambayo iko wazi kufuatia wajumbe wake kujiuzulu.

Kamati kuu ya chama hicho ilijiuzulu Jumapili kufuatia matamshi ya mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete kuwa kuna umuhimu wa chama hicho kujivua gamba ili kiweze kurejesha heshima yake mbele ya macho ya watu.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hili kujitokeza katika chama hicho kilichoanzishwa mwaka 1977.

Katika mkutano wa Halmashauri kuu ya Taifa unaomalizika leo mjini Dodoma, ajenda kuu iliyobakia ni kujaza nafasi zilizoachwa wazi na Kamati hiyo.

Mwandishi Kuringe Mongy akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka Dodoma anasema, “Kumekuwa na mtikisiko mkubwa wa kisiasa ndani ya chama ukizingatia kashfa za ufisadi, ukizingatia chama hiki kimepoteza viti kadhaa katika uchaguzi ulopita, kwa hiyo wameona kwamba waanze kuchukua hatua za haraka ili kuwa tayari kwa mkutano mkuu ujao mwakani kuweza kuchagua viongozi wepya.”

XS
SM
MD
LG