Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:14

Kikwete afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri


Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete

Kikao kijacho cha bunge kitakuwa na sura mpya za mawaziri na manaibu waziri kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete, Ijumaa

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kufuatia shutuma za matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa bungeni karibuni.

Rais Kikwete amewatangaza mawaziri wapya katika Wizara ya Ujenzi ni John Magufuli, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa-Shamsi Vuai Nahodha, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii-Hussein Mwinyi, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi-Shukuru kawambwa, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto-Sophia Simba, Wizara ya Maliasili na Utalii-Khamis Kagasheki, Wizara ya Viwanda na Biashara-Abdallah Kigoda, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo-Fenella Mukangara, Wizara ya Fedha-William Mgimwa na Wizara ya Nishati na Madini-Sospeter Muhongo..

Mawaziri wengine ni Bernard Membe-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria-Mathias Chikawe, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi-Emanuel Nchimbi, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi-David M.David, Wizara ya Kazi na Ajira-Gaudensia Kabaka, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia-Makame Mbarawa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi-Anna Tibaijuka, Wizara ya Maji-Jumanne Maghembe, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika-Christopher Chiza na Wizara ya Uchukuzi-Harrison Mwakyembe.

Rais pia amewatangaza manaibu waziri katika wizara mbali mbali, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira-Makongoro Mahanga, Naibu Waziri Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika-Adam Malima, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi-Pereira Silima, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi-Benedict Ole-Nangoro, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara-Gregory Teu, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto-Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi-Philipo Mulugo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii-Lazaro Nyalandu.

Manaibu waziri wengine ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki- Abdulla Juma Abdulla, Naibu Waziri wa Ujenzi-Gerson Lwenge, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii- Seif Suleiman Rashid, Naibu Waziri wa Nishati na Madini-George Simachawene, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia-Januari Makamba, Naibu Waziri wa Uchukuzi-Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo-Amos Makala, Naibu Waziri wa Maji-Binilith Mahenge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini-Stephen Maselle, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria-Angela Jasmine Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha-Janet Mbene na Naibu Waziri wa fedha-Saada Mkuya salum.

Taarifa inasema mawaziri hawa wataapishwa Mei 7 mwaka huu.

Hatua hii inafuatia baada ya baadhi ya wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa kutoka upande wa upinzani kuzusha mjadala mkali uliowashutumu baadhi ya mawaziri kutumia madaraka vibaya na ufujaji wa fedha za umma.

Wabunge waliwataja mawaziri hao kwa majina na kuwataka wajiuzulu kwa ridhaa yao au Rais kuwachukulia hatua. Pia walipiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu wa Tanzania bwana Mizengo Pinda.

XS
SM
MD
LG