Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:43

Tanzania: Mchungaji adai kuponya magonjwa sugu


Maelfu na maelfu ya watu wakikusanyika kwa Mchungaji Ambilikile kunywa dawa maalum ya kutibu magonjwa sugu.
Maelfu na maelfu ya watu wakikusanyika kwa Mchungaji Ambilikile kunywa dawa maalum ya kutibu magonjwa sugu.

Askofu Ambikile Mwasapile wa Tanzania adai Mungu amemwongoza kupata tiba ya magonjwa sugu

Wizara ya afya ya Tanzania na taasisi inayohusika na magonjwa ya binadamu nchini humo imeanza uchunguzi wa dawa inayodaiwa kuponya ukimwi, saratani, pumu na magonjwa mengine sugu, baada ya mchungaji mmoja kwa jina Ambilikile Mwasapile wa kanisa la kiinjili la kiluteli Tanzania (KKKT) kaskazini mwa nchi hiyo kudai kuwa amepata ndoto kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya dawa itakayoponya watu magonjwa hayo.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania Mussa Juma,aliiambia Sauti ya Amerika kuwa alikwenda kumhoji askofu huyu baada ya taarifa kujitokeza kuwa watanzania kutoka kila pembe ya nchi na hata wakenya wanakwenda kwa maelfu kupata dawa ya askofu Mwasapile.

Mahojiano na Mussa Juma

Juma aliiambia VOA kuwa aliwakuta hata mawaziri wa serikali, wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa na watu mashuhuri ambao walikuwa katika kijiji hicho cha Samunge katika wilaya ya Ngorongoro wakitafuta dozi hiyo anayotoa askofu huyo.

Mchungaji huyo anadai kuwa tangu mwaka jana alipewa ndoto na Mungu na kuonyeshwa mti ambao una dawa inayoweza kutibu wagonjwa wa Ukimwi, saratani, pumu na magonjwa mengine. Askofu huyo ametengeneza dawa hiyo ambayo anasema mtu anahitaji kunywa dozi ya kikombe kimoja tu na kuamini atapona na wala hakuna haja ya kupewa dawa zaidi.

Kufuatia wimbi la watu wanaokwenda kwa mchungaji huyo, serikali ya Tanzania, imeanza kuchunguza madai hayo kubaini ikiwa dawa hiyo kweli inatoa tiba au askofu anajitafutia umaarufu tu. Hadi tukienda hewani matokeo ya uchunguzi bado yalikuwa hayajatolewa.

Lakini mwandishi wa gazeti hili la Mwananchi,anasema serikali ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa, kwani kuna uwezekano wa kulipuka ugonjwa wa kuambukiza, kwa sababu watu wanaokwenda kwa mchungaji huyo ni wengi kuliko huduma za kimsingi zinazopatikana katika eneo hilo.

Bw. Juma anasema baadhi ya watu wameowaondoa wagonjwa wao hospitali kwa kuamini kuwa dawa ya askofu Mwasapile inaponya. Unaweza kufuatilia maelezo zaidi kwa kusikiliza mahojiano zaidi ya sauti ya Amerika.

XS
SM
MD
LG