Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:54

Wanaokabiliwa na njaa Syria wapokea msaada wa chakula.


Msururu wa magari yanayoelekea mji wa Madaya Syria
Msururu wa magari yanayoelekea mji wa Madaya Syria

Kiongozi wa upinzani George Sabra, aliambaia televisheni ya Al Arabiya kuwa serikali inatumia njaa kama sera, kote nchini na kwamba hicho ni kitendo kiovu.

Malori manne ya kwanza yanayopeleka misaada ya chakula na dawa, yamewasili mji ulozungukwa na kudhibitiwa na wapiganaji wa upinzani wa Syria, wa Madaya, ulio karibu na mpaka na Lebanon. Msafara mwengine wa malori unaripoti kuwa uko tayari kuingia miji ya Kefraya na Foua inayoshikiliwa na seriklai katika jimbo la Kaskazini Idlib.

Kituo cha televisheni cha Al Arabiya kilionyesha video ya malori manne ya kwanza kati ya msafara wa malori 70 ya misaada yakiingia Madaya. Msafara huo uliondoka mji mkuu wa Syria Damascus jana, kuelekea maeneo mawili yanayoshikilikwa nchini humo, eneo moja linashikiliwa na upinzani na linguine lnashikiliwa na serikali.

Rami Abdel Rahman, mkuu wa kundi la haki za binadam lenye makao yake mjini London la Syrian Observatory for Human Rights, aliambia , vyombo vya habari vya kiarabu kuwa msafara wa malorii 70 ya misaada unasafiri kwa wakati mmoja kuelekea sehemu zote mbili.

Anasema kati ya malori 70, 49 kati yao yalikuwa yanaelekea kwenye mji wa upinzani wa Madaya, na magari mengine 21, yalikuwa yanaelekea kwenye miji inayodhibitiwa na serikali ya Kafraya na Foua. Anasema, Madaya ina takriban raia elfu 40 wakati mji wa Kafraya na Foua una watu takriban elfu 18 na wapiganaji elfu 4000.

Abou Hassan Al Malah, mkuu wa baraza la mji wa Madaya, aliiambia vyombo vya habari vya kiarabu, kuwa msururu wa magari ya msada awali ulicheleweshwa kwenye kituo cha ukaguzi cha Hezbollah nje ya mji.

Anasema kuwasili kwa msaada huo kunatokana na kwamba msaada kama huo umepelekwa katika maeneo ya washia yanayoshikiliwa na serikali. Akiongeza kusema maafisa wa huko watasambaza msaada kwa usawa kwa wakazi wa mji, ambao ni wachovu na wanajaa, lakini kuna msaada tu wakutosha siku kumi.

Televisheni ya Al Manar ya Hezbollah, awali ilikana kuwa msafara huo ulisimamishwa.

Kiongozi wa upinzani George Sabra, aliambaia televisheni ya Al Arabiya kuwa serikali inatumia njaa kama sera, kote nchini na kwamba hicho ni kitendo kiovu.

Nadim Shehadi ambaye anaongoza kituo cha Fares Centre kwenye chuo cha Tufts, aliiambia sauti ya America kuwa jumuiya ya kimataifa inaikubalia tabia hiyo kutendeka.

Bw Shehadi anasema, jumuiya ya kimatifa inashirikiana na sera hii ya njaa, na mwakilishi wa zamani wa umoja mataifa kwa Syria, Lakhdar Brahimi, alisema bayana kuwa hatohusika katika jambo hilona akaacha kushirikiana. Brahimi alisema haya si maridhiano au usitishaji mapigano, lakini ni vita, na tunashirikiana na vita na kutumia mbinu za kivita.

Riyadh Hijab, anayeongoza kamati ya majadiliano upande wa upinzani , kwa ajili ya mazungumzo na serikali yaliyopangwa kufanyika huko Geneva baadaye mwezi huu, anasisitiza mazungumzo hayatofanyika hadi msaada wa chakula umepelekewa kwenye miji iliozungukwa nchini .

Vyombo vya habari vya kundi la Hezbullah ambalo linapigana ndani ya Syria kusaidia serikali, ilidai kuwa video na picha za watu walokumbwa na njaa ndani ya mji wa Madaya, kwa hakika zinatokea miji mengine ya nchi hiyo, na kwamba si jambo jipya.

XS
SM
MD
LG