Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:42

Zaidi ya watu millioni 5 wahitaji msaada Sudan


Zaidi ya watu milioni tano nchini sudan wanahitaji msaada wa haraka baada ya kukoseshwa makazi kwa karibuni huko Darfur na na ongezekol a wakimbizi wanaowasili kutoka Sudan kusini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ufaransa – AFP – mkurugenzi wa operesheni katika tume ya ulaya anayehusika na masuala ya kibinadamu na ulinzi wa raia, Jean Louis de Brouwer amesema baada ya tume kutoa msaada wa dolla milioni 14 kwa shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula duniani ili kusaidia katika operesheni za misaada nchini sudan.

De Brouwer amesema katika taarifa ya WFP kuwa hali ya kibinadamu katika sehemu za sudan ni mbaya, na watu waliokoseshwa makazi hivi karibuni huko Darfur na ongezeko la wale wanaowasili kutoka sudan kusini inajibainisha wazi.

Zaidi ya watu milioni tano wanahitaji msaada wa haraka ameongezea.

Mwishoni mwa mwezi april wfp ilisema ilikabiliwa na upungufu wa dola milioni 181 kwa kipindi cha miezi 12 ijayo, hali ambayo itadumazaz shughuli zake nchini sudan, hasa kwa wakimbizi wa sudan kusini.

Idara hiyo ya umoja wa mataifa imesema pia itatumia sehemu ya msaada huo kwa ajili ya kuwasaidia watu elfu 88 waliokoseshwa makazi kote Darfur kwa kuwapatia vocha kwa ajili ya chakula kwa kipindi cha miezi mitatu.

XS
SM
MD
LG