Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 08:36

Sudan yatakiwa ichunguze uhalifu unaotendwa kwa raia


Rais wa Sudan Omar al-Bashir
Rais wa Sudan Omar al-Bashir

Enough Project imeitaka serikali ya Sudan kufanya uchunguzi kwa raia wake wanaotendewa uhalifu

Kundi moja la kutetea haki za binadamu linasema majeshi ya Sudan yanauwa na kuwabaka raia katika jimbo la Blue Nile.

Kundi hilo kwa jina Enough Project limekariri mwito wake Jumanne uchunguzi ufanyike kuhusiana na uhalifu unaotendwa kwa raia katika jimbo hilo ambapo serikali ya Sudan imekuwa ikipigana na waasi tangu mwezi Septemba.

Kundi hilo la kutetea haki za binadamu lenye makao yake Marekani na ambalo linaungwa mkono na mcheza sinema maarufu George Clooney, linasema ripoti yake inafuatia mahojiano yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi oktoba na wakimbizi wa Ethiopia wanaoishi Blue Nile.

Kundi linawanukuu wakimbizi hao wakielezea jinsi majeshi ya Sudan yalivyowakimbiza raia katika mji wa Um Darfa na ‘kuwachinja’ baadhi yao. Mkimbizi mwingine alieleza jinsi wanamgambo wanaoiunga mkono serikali walivyowakamata baadhi ya wanawake mjini humo na kuwabaka.

Wakimbizi hao wanasema wanaamini walilengwa kutokana na rangi yao nyeusi. Kuna ripoti pia kuwa Sudan ilizuia misaada ya kibinadamu katika jimbo la South Kordofan ambapo pia inapigana na waasi. Majimbo yote mawili yamo kwenye mpaka wa Sudan Kusini ambayo ilijitenga na Sudan na kuwa taifa huru mwezi Julai.

XS
SM
MD
LG