Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:34

Sudan kuwa na sarafu mpya.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa kaskazini Omar al Bashir kwenye uwanja wa ndege wa Juba.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa kaskazini Omar al Bashir kwenye uwanja wa ndege wa Juba.

Rais al Bashir atangaza bungeni kutoa sarafu mpya ambayo huenda ikawa ni paundi ile ile lakini inayowakilisha Sudan kaskazini pekee

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema nchi yake itatoa sarafu mpya kufuatia kujitenga kwa upande wa kusini wiki iliyopita. Rais Bashir alitangaza mpango huo alipohutubia bunge mjini Khartoum Jumanne.

Sudan Kusini ilitangaza uhuru wake rasmi Jumamosi iliyopita na Jumatatu ikatangaza mipango ya kuwa na sarafu yake mpya.

Sarafu mpya ya Sudan Kusini inategemewa kuwasili kwa ndege ya mizigo kutoka Uingereza Jumatano na kuanza kuingizwa kwenye mzunguko wa fedha Jumatatu ijayo.

Haikujulikana mara moja ni wakati gani Sudan (Khartoum) itakuwa na sarafu mpya.

XS
SM
MD
LG