Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 09:52

Sudan Kusini yamshutumu Rick Machar kufuatia mauaji ya wafanyakazi wa UN


Ndugu wa wafiwa wanasubiri kuchukua miili ya ndugu zao waliouawa katika shambulio la Sudan Kusini.
Ndugu wa wafiwa wanasubiri kuchukua miili ya ndugu zao waliouawa katika shambulio la Sudan Kusini.

Naibu msemaji wa kijeshi wa upinzani SPLA-IO amesema kwamba eneo yalipotokea mauaji hayo iko chini ya udhibiti wa serikali na majeshi ya ushirika.

Wafanyakazi sita waliokuwa wanatoa misaada waliuawa Jumamosi wakati wakisafiri kutoka Juba kwenda Pibor.

Washambuliaji wasiojulikana waliwaua wafanyakazi sita Jumamosi ikiwa ni idadi kubwa ya watu kuuawa katika tukio moja tangu Sudan Kusini kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013 kwa mujibu wa Umoja wa mataifa.

Wakifanya kazi na taasisi isiyo ya kiserikali katika eneo hilo GREDO, waliuawa katika eneo la Magrio la jimbo la kati la Equatorial .

Jerry Ferrel mwakilishi wa huduma za kikatoliki wa Sudan Kusini amesema haamini kama makundi haya yanalengwa kisiasa. Badala yake anasema inawezekana wanatengwa kwa sababu zile zile ambazo wale wanaofikiriwa kuwa matajiri wanafanyiwa.

Kwa sababu taasisi zisizo za kiserikali zina magari makubwa ya Landcruiser na simu za satellite na mara zote wanabeba fedha taslim kwa ajili ya kufanya malipo kwa wale wanaowahudumia basi wanalengwa na wahalifu” aliongeza Ferrel.

Lakini Ken Isaacs makamu rais wa program na mahusiano ya serikali katika kituo chenye makao yake Marekani Samaritan’s Purse amesita kueleza sababu zozote.

"Kwa hiyo kuna vitu vingi na ninajua kutokana na uzoefu wangu wa kufanya kazi miaka 30 kwamba bado ni mapema sana kufikiria jambo lolote kuhusu suala hili.

, lakini ni mara chache sana kuwa rahisi kama inavyoonekana kwa juu juu" alisema Bw.Isaacs.

Serikali ya Sudan Kusini iliiambia VOA kwamba wanaohusika na mauaji haya ni askari wanaomuunga mkono kiongozi wa upinzani na makamu rais wa zamani Rick Machar .

Naibu msemaji wa kijeshi wa upinzani SPLA-IO aliiambia VOA kwamba eneo yalipotokea mauaji hayo liko chini ya udhibiti wa serikali na makundi ya ushirikiano ya kijeshi.

Samaritan Purse ina wafanyakazi 15 waliotekwa nyara huko Mayendit kati kati ya Machi na kundi la kijeshi linalojitegemea lakini wote hao waliokolewa muda mfupi baadae.Isaacs anasema shambulizi hilo la mwishoni mwa juma litafanya shirika yake ifanye kazi kwa uangalifu mkubwa.

Shambulizi hilo halitazuia jumuiya ya kimataifa ya msalaba mwekundu kusafirisha misaada huko Sudan Kusini alisema msemaji Jason Straziuso.

Hili ni tukio baya sana ni jambo lililo juu kabisa katika ajenda yetu kwa sasa imeongezeka katika wasi wasi wa usalama Sudan Kusini . Lakini wakati huo huo kwa jinsi tunavyofanya kazi kwasababu wakati mwingi tunasafiri na ndege hii haitaathiri sana operesheni zetu za msaada wa chakula au msaada wa matibabu .Tutaweza kufanya haya kwa sababu ya njia ya usafiri tunayotumia.

Ferrell wa Catholic Relief Services anasema mauaji hayo yameendelea kuwapa nguvu taasisi zisizo za kiserikali zinazofanya kazi huko Sudan Kusini.

"Tunaongeza juhudi zetu mara mbili zaidi .Haopana nafikiri hii ni kwa kila mtu. Ni masikitiko makubwa kwetu lakini kila mtu ana moyo mkubwa zaidi wa kusaidia watu ambao wako katika shida kubwa ya misaada" alisema Ferell.

Tume ya Sudan Kusini ya usimamizi na ukaguzi wamewaomba wasimaimizi wa sitisho la mapigano la mwaka 2015 kuchunguza tukio hilo.

Umoja wa mataifa unasema tangu Desemba 2013 wafanyakazi wapatao 79 wa misaada wameuwawa Sudan Kusini ikiwa ni pamoja na 12 mwaka huu.

XS
SM
MD
LG