Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:46

Sudan Kusini kujiunga na Umoja wa Mataifa


Watu kadhaa wakimpokea rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipokuwa akiwasili nyumbani.
Watu kadhaa wakimpokea rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alipokuwa akiwasili nyumbani.

Rais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa asema baraza hilo lategemea kupendekeza uanachama wa Sudan Kusini.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa anasema Sudan Kusini inaweza kujiunga rasmi na umoja wa mataifa mapema iwezekanavyo hata wiki ijayo.

Taifa hilo jipya ambalo litajulikana kama Jamhuri ya Sudan Kusini linajiandaa kusheherekea uhuru wake Jumamosi.

Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa Peter Wittig ambaye ndio rais wa baraza hilo kwa mwezi huu, amesema Jumanne kuwa anategemea baraza la usalama kupendekeza uanachama wa Sudan Kusini ifikapo July 13. Alisema Baraza Kuu linategemewa kupiga kura siku itakayofuata.

Kama wakipitishwa Sudan Kusini litakuwa taifa mwanachama la 193 kwenye Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Mataifa pia unafikiria kuunda tume mpya ya kulinda amani huko Sudan Kusini.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ataapishwa Jumamosi baada ya kusaini katiba mpya ya mpito nchini humo.

XS
SM
MD
LG