Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:12

Sudan Kusini yalaumiwa kutumia siasa za ukabila


Mwanamke mmoja akikimbia kuokoa maisha yake baada ya shambulizi la anga huko Sudan Kusini. April 23, 2012. (Reuters).
Mwanamke mmoja akikimbia kuokoa maisha yake baada ya shambulizi la anga huko Sudan Kusini. April 23, 2012. (Reuters).

Serikali ya Sudan Kusini na majeshi yake yamelaumiwa kwa kuwalenga kimfumo wananchi wake kwa misingi ya kikabila.

Yasmin Sooka aliliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kwamba raia wamekuwa wakilengwa kimfumo kwa sababu ya kabila zao na serikali ya nchi hiyo na majeshi yake.

Kumekuwa na ongezeko kubwa katika ukiukaji wa haki za binadamu huko Sudan Kusini katika miezi tisa iliyopita na sehemu ni kutokana na kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kuunda mahakama na kuwafikisha wakosaji mbele ya sheria afisa mmoja wa Umoja wa mataifa alieleza.

"Ukubwa wa ukosefu wa haki za binadamu huko Sudan Kusini hasa ghasia za ngono ni mbaya sana kiasi kwamba matokeo ya kutofanya lolote huwezi hata kufikiria yatakuwaje" mwenyekiti wa tume ya Umoja wa mataifa ya haki za binadamu huko Sudan kusini alisema.

Yasmin Sooka aliliambia baraza la haki za binadamu la Umoja wa mataifa huko Geneva siku ya Jumanne kwamba raia wamekuwa wakilengwa kimfumo kwa minajili ya kabila zao na serikali ya nchi hiyo na majeshi yake. Anasema serikali imeanza kampeni ya kufuatilia wakazi na kuwafuatilia watu kutokana na kabila zao wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vikiendelea huku kukiwa na maonyo ya mauaji ya haliki.

XS
SM
MD
LG