Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 12:26

Serikali ya Sudan na kundi moja la uasi watia saini


Rais wa Sudan Omar al-Bashir
Rais wa Sudan Omar al-Bashir

Serikali ya Sudan na kundi moja la uasi mkoani Darfur wametia saini mkataba wa amani uliokataliwa na makundi makuu ya uasi katika mkoa huo.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC kwa mashtaka ya uhalifu wa vita katika mkoa wa Darfur alihudhuria sherehe za kutia saini huko Doha, Qatar hapo Alhamis.

Serikali iliingia mkataba na kundi la Justice and Liberation Movement-JLM kundi lililoundwa na makundi ya uasi yaliyojitenga. Msemaji wa kundi kubwa la uasi mkoani Darfur la Justice and Equality Movement-JEM amesema mkataba huo hautatui matatizo makuu ya Darfur.

Msemaji wa JEM, Gibree Adam Bilal, amesema matatizo hayo yakiwemo ukiukaji wa haki za binadamu, mgao wa madaraka na utajiri na fidia na kurudi kwa watu waliopoteza makazi hayo. Marekani ilisema makubaliano hayo ni hatua nzuri ya kusonga mbele yenye matumaini katika kupatikana kwa suluhisho la kudumu kwa matatizo.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Mark Toner alisema Marekani itaendelea kuwashinikiza waasi wa Darfur ambao wanakataa kushiriki katika mashauriano kujihusisha kikamilifu katika uaratibu wa amani.

Msemaji pia aliisihi serikali ya Sudan kuwa wazi kwa mashariano zaidi ya kimataifa ili mkataba wa amani uweze kufikiwa na makundi yote ya uasi huko Darfur.

Mazungumzo ya amani yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa huko Qatar kati ya waasi wa Darfur na serikali ya Sudan yameonyesha mafanikio kiasi.






XS
SM
MD
LG