Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 17, 2024 Local time: 02:53

Mapambano Sudan Kusini yasababisha dazeni ya vifo


Wakazi wa Agok wakiwa chini ya mti kwenye mahakama ya kijadi katika eneo lenye mzozo la Abyei huko Sudan kusini
Wakazi wa Agok wakiwa chini ya mti kwenye mahakama ya kijadi katika eneo lenye mzozo la Abyei huko Sudan kusini

Maafisa huko Sudan kusini wanasema mapambano katika maeneo mawili muhimu yamesababisha dazeni ya vifo vya watu.

Katika ghasia za karibuni,wanamgambo katika eneo lenye mzozo la Abyei kuhusu mpaka kati ya kaskazini-kusini walipigana Jumatano na polisi wa kusini.

Maafisa wanasema watu wasiopungua sita waliuwawa. Mapigano pia yalitokea Jumapili kati ya jeshi la Sudan kusini na majeshi ya kiongozi muasi wa jeshi wa mkoa wa kusini wa Fangak, katika jimbo la Jonglei.

Kiongozi wa uasi, George Athor, anasema kwamba majeshi yake yaliwauwa zaidi ya wanajeshi 80 na yalichukua idadi kubwa ya silaha. Msemaji wa jeshi la Kusini, Philip Aguer, alisema Athor anakuza idadi ya vifo lakini alithibitisha kuwepo mapigano na alikiri kwamba wanajeshi 40 wa Kusini waliuwawa.

Athor, afisa mwandamizi wa zamani wa jeshi la taifa alianzisha uasi wake mwaka jana baada ya kushindwa uchaguzi wa nafasi ya gavana katika jimbo la Jonglei.



XS
SM
MD
LG