Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 07:02

Serikali ya Somalia kuwarejesha nyumbani wakimbizi walioko Kenya


Wakimbizi wa kisomalia wakisuburi ndege ya kuwarejesha nyumbani kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo kaskazini mwa Kenya.(Februari 21, 2000).
Wakimbizi wa kisomalia wakisuburi ndege ya kuwarejesha nyumbani kutoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo kaskazini mwa Kenya.(Februari 21, 2000).

Maafisa wa Somalia wanasema wanatarajia kuwarejesha kwa awamu zaidi ya wakimbizi wa kisomali 300,00 kutoka Kenya katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Maafisa wanasema ni watu 5,500 tu hadi hivi sasa wamerejea nchini, lakini wanatarajia kwamba idadi hiyo itafikia 12,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu, na kuongezeka mpaka 75,000 idadi ya wanaotarajiwa kurejesha nyumbani mwaka ujao.

Maafisa wanasema wanapanga kwamba wakimbizi wote 320,000 wa kisomali watarejea nchini ifikapo mwaka 2019.

Tangazo hilo limekuja baada ya Waziri Mkuu wa Somalia, Omar Abdirashid Sharmake kutembelea kambi za wakimbizi siku ya Ijumaa nchini Kenya.

Kiongozi aliyemtangulia Abdiweli Sheikh Ahmed alizitembelea kambi hizo mwaka mmoja uliopita.

Sharmake anasema ziara hiyo inaonyesha wasi wasi wa serikali kuhusu hatima ya muda mrefu ya wakimbizi hao, wengi wao wamekimbia nchini takriban miaka 25 iliyopita. Amesema serikali yake inafanya kazi kuhakikisha kuwa mazingira ni mazuri kwa wao kurejea nyumbani.

Katika mkutano wa karibuni uliofanyika mjini Brussels, wafadhili waliahidi msaada wa takriban dola milioni 500 kuwarejesha wakimbizi, lakini maafisa wanasema hadi hivi sasa wamepata dola milioni 105 tu.

XS
SM
MD
LG