Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 17:32

Tufani ya theluji yakumba Mashariki mwa Marekani


Theluji katika mji wa Alexandria, Virginia katika picha hii iliyopigwa tarehe 23 Januari, 2016. T
Theluji katika mji wa Alexandria, Virginia katika picha hii iliyopigwa tarehe 23 Januari, 2016. T

Na BMJ Muriithi

Tufani ya Theluji na barafu inaendelea kuathiri maeneo kadhaa ya pwani ya Mashariki mwa Marekani, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Washington DC. Theluji ilianza kuanguka ijumaa alasiri na hali hii inatarajiwa kuwa mbaya hata Zaidi kufikia Jumamosi usiku na kuendelea hadi usiku wa kuamkia Jumatatu.

Inatarjiwa kwamba theluji itafikia kiwango cha Zaidi ya futi 3 katika maeneo mengine. Wataalamu wa maswala ya hali hewa wamesema kwamba hali hii itaingia kwenye historia kama moja ya tufani mbaya Zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Marekani.

Mamlaka ya hali ya hewa mjini Washington imewashauri wananchi wote kukaa nyumbani na kuwaonya wale wanaoendesha magari kwenye barabara za mji huo na majimbo ya Virginia na Maryland kwamba wanahatarisha maisha yao.

Imetabiriwa kuwa tufani hii itaathiri takriban watu milioni themanini na tano kwa njia moja au nyingine.

“Hili ni swala la kufa na kupona,” alisema meya wa mji wa Washington, Muriel Bowser siku ya Ijumaa.

Kufikia Jumamosi asubuhi, maelfu ya watu walikuwa wamepoteza umeme kwenye nyumba zao baada ya miti iliyopata uzito mwingi kutokana na barafu kuangukia vikingi vya stima kwenye maeneo mengi.

Vile vile watu wanaoishi maeneo ya New Jersey, kuelekea Philadelphia, New York, Massachusetts na New Hampshire walionekana wakijitayarisha baada ya idara ya hewa kutangaza kwamba tufani kubwa ya theluji na barafu itafika maeneo hayo siku Jumamosi.

Safari za ndege katika anga za maeneo yaliyoathiriwa zimesitishwa kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa. Hii imeathiri usafiri katika mamia ya miji ya Marekani, hata ingawa baadhi ya miji hiyo haijakumbwa na hali hiyo mbaya ya hewa.

Tayari watu nane wameripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na hali hiyo, huku wanne wakiwa ni wakazi wa jimbo la North Carolina. Hata hivyo, mamlaka hazijatoa habari rasmi kuhusu jinsi watu hao walivyopoteza maisha yao.

Shirika la utangazaji la CNN lilitangaza Ijumaa usiku kwamba rais wa Marekani Barack Obama alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa makini akiwa kwenye ikulu ya White House.

XS
SM
MD
LG