Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:56

Sitisho la mapigano nchini Syria huenda likatangazwa karibuni


Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov(kushoto) akiwa na mwakilishi wa Umoja wa Maaifa kwa Syria, Staffan de Mistura mjini Moscow.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov(kushoto) akiwa na mwakilishi wa Umoja wa Maaifa kwa Syria, Staffan de Mistura mjini Moscow.

Waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov amesema Jumanne kwamba sitisho la mapigano huenda likatangazwa katika hivi punde kati ya waasi na majeshi ya serikali huko Aleppo, syria hata wakati ambapo mapambano mapya yamesababisha vifo vya watu 14.

Mwanadiplomasia wa Russia amekutana mjini Moscow na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Staffan de Mistura, na kuwaeleza waandishi wa habari kuwa alikuwa na matumaini kwamba sitisho la mapigano huenda likafikiwa " katika siku chache zijazo au hata saa chache".

Mapigano yamekuwa mabaya sana kuzunguka mji wa kaskazini wa Aleppo ambako mashambulizi ya anga ya serikali na waasi yameuwa mamia ya watu katika kipindi cha wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG