Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:25

Jeshi la Marekani: Shambulio dhidi ya Syria laonyesha mafanikio


Shambulio la makombora ya Jeshi la Marekani nchini Syria
Shambulio la makombora ya Jeshi la Marekani nchini Syria

Jeshi la Marekani limeshambulia Syria kwa makombora mapema Ijumaa ikiwa ni kulipiza kisasi kitendo cha nchi hiyo kutumia silaha za kemikali kwa wananchi wake.

Hatua hiyo inatokana na kitendo cha majeshi ya Rais Bashar al-Assad yanayo endelea kulaumiwa na ulimwengu mzima kwa kusababisha vifo vya takriban watu 100.

Hili ni shambulio la kwanza la moja kwa moja dhidi ya vikosi vya serikali ya Syria.

Russia yalaani shambulizi hilo

Russia, ambayo imepeleka vikosi vyake na msaada wa jeshi la anga kwa Serikali ya Assad, wamelaani mashambulizi yaliofanywa na Marekani, wakisema ni “uvunjifu wa amani dhidi ya nchi huru,” na kusema inasitisha makubaliano yaliyofikiwa na Marekani kuhusu kuwepo maeneo salama kurusha ndege zake katika anga la Syria.

Manuari aina ya destroyer USS Porter ya Jeshi la Majini la Marekani imetuma makombora aina ya Tomahawk kutoka Bahari ya Mediterranean, April 7, 2017. Marekani imekishambulia kiwanja cha ndege cha Syria kwa makombora ya nguvu kwa kulipiza kisasi kitendo cha Syria kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia wiki hii.

Makombora 59 ya aina ya Tomahawk yalifyatuliwa wakati wa saa 4:40 asubuhi kutoka katika meli za kivita ya Marekani USS Ross na USS Porter, ambazo zimetia nanga katika mashariki ya bahari ya Mediterranean. Shambulizi hilo lilidumu kwa dakika tatu mpaka nne, maafisa wa Marekani wamesema.

Vikosi vya Marekani vinasemekana kuwa vililenga mashambulizi yake katika uwanja wa ndege wa Shayrat huko magharibi ya Syria. Afisa wa Jeshi la Majini ameiambia VOA kuwa uwanja wa ndege huo ulilengwa kwa sababu kuna uwezekano mkubwa ulitumika kufanya shambulio la Kemikali dhidi ya eneo la wapinzani Jumanne.

Kutumika kwa gesi ya Sarin

Baadhi ya watu walioathirika na silaha za kemikali zilizotumiwa na Rais Assad wa Syria.
Baadhi ya watu walioathirika na silaha za kemikali zilizotumiwa na Rais Assad wa Syria.

“Tunaamini kwa kiwango kikubwa kwamba shambulio hilo lilikuwa limefanywa na ndege iliopewa amri kutekeleza hilo na utawala wa Bashar al-Assad.

Tunaamini kwa kiwango kikubwa kuwa shambulio hilo lilitumia aina ya gesi ya sarin nerve, inayoshambulia mishipa ya fahamu,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amewaambia waandishi jioni Alhamisi.

Umuhimu wa shambulio la Marekani

Tillerson amesema ilikuwa muhimu kuchukua hatua dhidi ya kiongozi wa Syria, kwa sababu “ Assad ameendelea kutumia silaha za kemikali katika mashambulizi haya bila ya kuchukuliwa hatua, bila ya hatua yoyote kuchukuliwa na jumuiya ya kimataifa, yeye- kwa vitendo- anahalalisha utumiaji wa silaha za kemikali, kitu ambacho kinaweza kuja kuigwa na wengine.”

Hatua lazima zichukuliwe, amesema “ ilikuweka wazi kuwa silaha za kemikali hizi ni muendelezo wa uvunjaji wa utaratibu wa kimataifa.”

Mshauri wa Usalama wa Taifa HR McMaster amesema shambulizi hilo la Marekani liliepuka kupiga maeneo ya depo yaliyo katika Kituo cha kijeshi cha anga ya nchi hiyo ambapo maafisa wa Marekani wanaamini ndipo Kemikali ya Serin inapohifadhiwa.

“Bila ya shaka, serikali itaendelea kuwa na nguvu kufanya vitendo vya mauaji ya halaiki kwa kutumia silaha za kemikali hata nje ya uwanja wa ndege,” McMaster amesema. Lakini, ameongeza kuwa, “Hili halikuwa shambulizi dogo.”

Wizara ya Mambo ya Nje

Kapteni Jeff Davis
Kapteni Jeff Davis

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Kapteni Jeff Davis amesema maeneo yaliolengwa na shambulizi hilo ni uwanja wa ndege, majengo, depo za mafuta na bohari za serikali na sehemu za siri za kuhifadhi silaha.

“Matokeo ya kwanza baada ya shambulizi hili la Marekani yanaonyesha kuwa limekuwa na athari kubwa au limeangamiza ndege za Syria na miundo mbinu yake na vifaa katika uwanja wa ndege wa Shayrat, ikipunguza uwezo wa jeshi la Syria kutumia silaha za kemikali,” Davis amesema katika tamko lake.

Tillerson ameongeza kusema, “Tunahisi kuwa shambulizi hili peke yake lilikuwa linajitosheleza kwa sababu lilielekezwa katika vifaa ambavyo vilitumika katika shambulizi la hivi karibuni kwa kutumia silaha za kemikali.”

XS
SM
MD
LG