Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:11

Mlipuko waua watatu Uturuki


Rais wa Uturuki
Rais wa Uturuki

Afisa wa polisi na raia wawili wameuawa baada ya bomu la kwenye gari kulipuka nje ya kituo cha polisi nchini Uturuki, karibu na mpaka wake na Syria, Waziri mkuu wa Uturuki, Binali Yil-dirim, amesema leo Jumatano.

Takriban watu 30 wameuawa na magari mengi ya kubebea wagonjwa yametumwa kwenye eneo la tukio hilo katika mji wa Midyat, ulio kwenye eneo la Kusini Mashriki lenye Wakurdi wengi.

Waziri mkuu Yil-dirim amewashutumu wanamgambo wa Kikurdi kwa shambulizi hilo. Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi, PKK, kimekuwa kikiwalenga polisi wa Uturuiki na wanajeshi tangu mwezi Julai mwaka jana katika mapambano yao ya kutaka uhuru katika eneo la Kusini Mashariki mwa Uturuki.

Waziri huyo Mkuu alizungumza baada ya kuwatembelea majeruhi mjini Istanbul ambako shambulizi linguine lilikuwa limetokea siku ya Jumanne, ambalo liliwaua watu kumi na mmoja, wakiwemo maafisa saba wa polisi, na kuwajeruhi watu wengine 36, wakati wa msongamano wa asubuhi.

XS
SM
MD
LG