Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:44

Mwanasheria Mkuu : 'Wakati ukifika nitajiuzulu au kujiondosha'


Jeff Sessions
Jeff Sessions

Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions amesema ikiwa “itabidi” atajiondasha katika uchunguzi unaofanywa na idara ya upelelezi juu ya mambo mengi yanayoihusu Russia katika madai ya kuingilia kati uchaguzi wa rais mwaka jana.

Hivi karibuni Seneta huyo wa zamani aliapishwa kuwa afisa msimamizi wa juu kabisa wa sheria, baada ya kuwa mtu wa karibu sana kati ya wafuasi wake Trump wakaribu wakati wa kinyang’anyiro cha kuingia White House.

Ametakiwa na baadhi ya wabunge kujiuzulu au angalau ajiondoshe katika upelelezi huo kwa sababu ya kukanusha kwake, wakati wa mahojiano ya kuthibitishwa katika wadhifa wake aliofanya na Seneti, mwezi Januari, kwamba hakuwa anajua mtu yoyote katika kampeni ya Trump aliyekuwa na mawasiliano na maafisa wa Russia.

Hata hivyo Wademokrati katika Bunge la Marekani wamemtaka Mwanasheria Mkuu kujiondosha kutoka kwenye uchunguzi unaohusu Russia kuvuruga uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba, au kujiuzulu, baada ya kujulikana kuwa Sessions alikutana mara mbili mwaka jana na balozi wa Russia nchini Marekani.

Sessions alimsaidia rais Donald Trump katika kinyang’anyiro cha urais na alikuwa ni mshauri wa kampeni yake wakati bado akitumikia katika Baraza la Seneti ya Marekani.

Baada ya kuteuliwa kuiongoza Idara ya Sheria, Sessions aliulizwa wakati wa mahojiano ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo Januari atafanya nini iwapo kutapatikana ushahidi kwamba mmoja wa waliokuwa katika kampeni ya Trump alikuwa na mawasiliano na Russia.

“Mimi nimeitwa mwakilishi wake mara moja au mbili katika kampeni ile na sijawahi kuwa hivyo, sijawahi kuwa na mawasiliano na Russia, na siwezi kulizungumzia hilo,” amesema.

Sessions alikutana na balozi Sergei Kislyak mwezi Julai wakati wa mkutano mkuu wa chama cha Republikan na tena Septemba huko ofisini kwake Capitol Hill.

Msemaji wa Idara ya Sheria Sarah Isgur Flores amesema “kulikuwa hakuna kitu chochote chenye kudanganya kuhusu kauli alioitoa Sessions alipokuwa anachukua kiapo wakati anathibitishwa.

Amesema aliulizwa kuhusu mawasiliano yaliyokuwapo kati ya Russia na Kampeni ya Trump, sio mikutano aliyofanya kama Seneta.

“Sikuwahi kukutana na afisa yoyote wa Russia kuzungumzia masuala ya kampeni,” Sessions amesema katika kauli yake ya baadae ambayo ilipostiwa kwenye Twitter na Flores. “Sijui kabisa madai haya yanahusu nini. Ni uongo.”

Shirika la Upelelezi la FBI, ambayo ni sehemu ya Idara ya Sheria, inachunguza vitendo vya Russia vilivyokuwa na nia ya kuvuruga uchaguzi wa Marekani na kuwepo uwezekano wa ushirikiano kati ya kampeni ya Trump na serikali ya Rais wa Russia Vladimir Putin.

Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti inafanya uchunguzi kwa upande wake, na kamati ya usalama ya Bunge imetangaza mipaka ya uchunguzi wao Jumatano.

Seneta Al Franken, ambaye alimuuliza Sessions suala linalohusu mahusiano na Russia wakati wa mahojiano ya kupitishwa kwake katika wadhifa huo, amesema:

“Kwa hivyo ni wazi kuwa haitawezekana kabisa kwa Mwanasheria Mkuu, kwa nia nzuri kabisa, kusimamia uchunguzi katika Idara ya Sheria na uchunguzi wa mahusiano ya Trump na Russia, na ni lazima ajiondoshe mara moja yeye mwenyewe katika uchunguzi huu.

Kiongozi wa Wademokrati ndani ya Bunge Nancy Pelosi ameenda mbali zaidi kutaka Sessions ajiuzulu.

“Sessions hawezi kuwa afisa mkuu wa kusimamia sheria katika nchi yetu na lazima ajiuzulu.

Lazima uchunguzi uwe huria na ushirikishe vyama vyote viwili nje ya tume kuchunguza mahusiano yake Trump kisiasa, kibinafsi na kifedha na Russia,” amesema Pelosi.

XS
SM
MD
LG