Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:00

Sudan kusini yashindwa kulipa malipo ya hoteli katika makazi ya waasi


Kiongozi wa upinzani, Riek Machar.
Kiongozi wa upinzani, Riek Machar.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini, Barnaba Marial Benjamin, anasema serikali imeanza kulipa malipo baada ya kundi la pamoja kwa nchi za Marekani, Uingereza na Norway.

Serikali ya Sudan Kusini inasema mwishoni mwa wiki hii itasitisha kulipa malipo ya hoteli ya kiasi cha wanachama wa uasi 600 ambao wamekuwa wakiishi mjini Juba tangu Disemba mwaka jana kwa ajili ya kufanya kazi ya utekelezwaji wa mkataba wa amani ulioafikiwa Agosti mwaka jana. Timu hiyo pia imekuwa ikifanya maandalizi ya kwenda Juba kwa kiongozi wa waasi, Riek Machar.

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini, Barnaba Marial Benjamin, anasema serikali imeanza kulipa malipo baada ya kundi la pamoja kwa nchi za Marekani, Uingereza na Norway yaani TROICA, pamoja na tume ya pamoja ya uangalizi na tathmini JMEC ambayo ilisitisha malipo yake. Benjamin anasema serikali haina tena uwezo wa kufanya malipo hayo.

XS
SM
MD
LG