Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:45

Serikali ya Sudan Kusini na waasi watia saini makubaliano


Raia wakitafuta sehemu salama kwa maisha yao baada ya mapigano kuzuka Sudan Kusini
Raia wakitafuta sehemu salama kwa maisha yao baada ya mapigano kuzuka Sudan Kusini
Serikali ya Sudan Kusini na upinzani wametia saini mikataba miwili alhamisi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mkataba wa kwanza ni sitisho la haraka la hatua za kijeshi na wa pili unahusu kuachiliwa kwa wafungwa 11 wa kisiasa ambao wametiwa ndani tangu kuanza kwa mzozo katikati ya mwezi Disemba mwaka uliopita.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mazungumzo ya amani yameongozwa na taasisi ya kieneo IGAD na yalianza mapema mwezi uliopita. Mpatanishi mkuu wa IGAD, Seyoum Mesfin anasema hatua kadhaa zinahitaji kuchukuliwa na pande zote kwa vile hivi sasa wametia saini mikataba miwili.

Bwana Seyoum anasema moja ni kutekeleza mikataba ambayo wametia saini kwa nia nzuri na ya dhati. Pili, kuanza kufanya kazi za ukarabati na kuwasaidia maelfu ya watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi na wakimbizi. Tatu, lazima tuendelee haraka na majadiliano ya kisiasa na kufanya kazi kuelekea katika maridhiano ya kitaifa.

Mkataba wa sitisho la mapigano unayataka majeshi ya serikali na upinzani kubakia walipo. Wanajeshi wa Uganda ambao wanaisaidia serikali ya Sudan Kusini itawalazimu waache operesheni zote katika muda wa saa 24.

Mkataba unaozungumzia wafungwa 11 haujaelezea wataachiliwa lini.Hakuna maneno ya kirafiki yaliyozungumzwa kati ya serikali ya Sudan Kusini na upinzani wakati wa sherehe za utiaji saini.
XS
SM
MD
LG