Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:29

Serikali ya Somalia yateka sehemu za mji mkuu

Majeshi ya serikali Somalia yakifanya doria.
Majeshi ya serikali Somalia yakifanya doria.

Serikali ya Somalia imesema majeshi yake yameteka baadhi ya sehemu za mji mkuu Mogadishu ambazo kwa muda mrefu zilishikiliwa na waasi wa Kiislam.

Serikali ya Somalia imesema majeshi yake yameteka baadhi ya sehemu za mji mkuu Mogadishu ambazo kwa muda mrefu zilishikiliwa na waasi wa Kiislam.

Maafisa wanasema mafanikio hayo yalitokana na mashambulizi ya majeshi ya serikali na yale ya umoja wa Afrika kwenye maeneo ya vikosi vya wanamgambo alshabab jumanne.

Wamesema moja ya maeneo yaliotekwa lilikuwa ni jengo la zamani la wizara ya ulinzi ambalo waasi wamelitumia kama ngome yao. Majeshi yanayounga mkono serikali yalipata mafanikio katika eneo la Shirkole.

Mwandishi mmoja huko Mogadishu ameiambia Sauti ya Amerika (VOA) kwamba watu 20 wameuwawa katika mapigano hayo na wengine 30 wamejeruhiwa.

Serikali imeshikila maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege na jumba la rais kwa msaada wa walinda amani wa Umoja wa Afrika kutoka Uganda na Burundi.

XS
SM
MD
LG