Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:59

Serikali ya Gambia imewahamisha wafungwa wa kisiasa nchini humo


Wanaharakati huko Gambia katika maandamano dhidi ya shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu.
Wanaharakati huko Gambia katika maandamano dhidi ya shutuma za ukiukwaji wa haki za binadamu.

Chama cha upinzani nchini Gambia, United Democratic Party (UDP), kimesema Jumatano kwamba serikali ya nchi hiyo imewahamisha wafungwa wa kisiasa ambao idadi yake haikutolewa na kuwapeleka sehemu isiyojulikana.

Wanachama 38 wa upinzani akiwemo kiongoizi wa UDP, Ousainou Darbo, walikamatwa mwezi uliopita, na kufunguliwa mashtaka kwa tuhuma za uhalifu baada ya kufanya maandamano kupinga kifo cha afisa wa chama hicho, Solo Sadeng, aliyefariki akiwa kizuizini pamoja na kuitisha mageuzi ya kisiasa.

Kiongozi wa upinzani nchini Gambia, Ousainu Darbo.
Kiongozi wa upinzani nchini Gambia, Ousainu Darbo.

Upinzani unadai kuwa serikali imewashikilia wafungwa hao wa kisiasa.

Mwenyekiti wa kitengo cha chama cha UDP kinachoshugulikia mawasiliano ya wa-Gambia wanaoishi katika nchi za nje, Karamba Touray, alisema kuwa chama chake kinaituhumu serikali ya Gambia kwa kuwashikilia wapinzani hao wa kisiasa na kwamba ni jukumu la serikali hiyo kuhakikisha usalama na afya njema kwa wafungwa hao wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG