Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:50

Serikali ya Cameroon yasema Rais Biya sio mgonjwa


Rais Paul Biya wa Cameroon akiwa na mkewe, Chantal Biya
Rais Paul Biya wa Cameroon akiwa na mkewe, Chantal Biya

Maafisa nchini Cameroon wanakanusha kwamba Rais Paul Biya mwenye umri wa miaka 82 ni mgonjwa sana. Waziri wa mawasiliano nchini Cameroon, Issa Tchiroma Bakary aliwaambia waandishi wa habari Jumanne kwamba Rais Biya ambaye yupo nje ya nchi tangu machi tatu kwa ziara binafsi huko ulaya na kwamba hakwenda kwa masuala ya afya yake kwenye hospitali ya Geneva kama ilivyoripotiwa.

“Mkuu wa nchi, mheshimiwa Paul Biya na mke wake kwa hivi sasa wapo katika ziara fupi binafsi huko ulaya na hali yao ya kiafya haina sababu ya kutiliwa mashaka hata kidogo. Rais wa Jamhuri pamoja na mke wake wanaendelea vizuri na salama”, Tchiroma alisema.

Kwa mujibu wa waziri huyo wa mawasiliano shutuma hizo zilitolewa kwanza na gazeti moja la Kifaransa la Le Monde. Aliziita sehemu za ripoti hizo ni kampeni za uongo dhidi ya bwana Biya.

“Wa-Cameroon sio wajinga wa mambo, wenye nia mbaya na njama za uchonganishi kuhusu mashambulizi haya yanayorejewa dhidi ya nchi yetu kupitia vyombo vya habari. Lakini taarifa hizi za kuumiza na uvumi mwingine usio na maana unatakiwa kuwa nao makini na kamwe usipewe nafasi kudumaza na kuhatarisha matarajio ya taifa la wa Cameroon na kiongozi wake kuongoza nchi kuelekea mafanikio na ukuaji wake,” alisema.

Rais Paul Biya, Jan 30, 2013.
Rais Paul Biya, Jan 30, 2013.

Hapo Juni mwaka 2004 kulizuka uvumi kwamba bwana Biya alifariki katika kliniki moja huko Uswisi. Mara aliporejea nchini Cameroon alisema kwenye televisheni ya taifa kwamba wale wanaomtakia kufa lazima wasubiri miaka mingine 20 ijayo.

XS
SM
MD
LG